30.5 C
Dar es Salaam
Monday, December 6, 2021

Wizara ya Afya yaanzisha dawati la kuratibu mashirika yasiyo ya Kiserikali

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeanzisha Dawati la kuratibu Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali kwa lengo kuboresha usimamizi wa Serikali katika shughuli zinazofanywa na mashirika hayo katika sekta ya afya.

Dk. Dorothy Gwajima amebainisha hayo leo Jumatatu Novemba 15, jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika lisilo la kiserikali la AMREF Tanzania, Dk. Florence Temu katika kikao cha kujadili miradi inayosimamiwa na shirika hilo kwa lengo la kuongeza ufanisi wenye tija na uwajibikaji.

Dk. Gwajima ameshukuru shirika la AMREF kwa kusimamia utekelezaji wa miradi ya afya toka shirika hilo liliposajiliwa rasmi hapa nchini. Aidha, amelipongeza shirika hilo kwa kushirikiana na Serikali katika kutekeleza vipaumbele vya kudhibiti UVIKO-19 katika ngazi ya jamii.

Awali akitoa taarifa kwa Gwajima, Mtendaji Mkuu wa Shirika la AMREF, Tanzania, amesema kuwa shirika limejipanga kushirikiana na Serikali kuboresha huduma za afya kwa wananchi kwa kuzingatia vipaumbele vya kimkakati na miongozo ya serikali.

Amesema kuwa AMREF inatekelezairadi miradi katika mikoa na Halmashauri zote nchini katija maeneo afya ya uzazi, mama na mtoto, kuzuia na kudhibiti magonjwa,kuwajengea uwezo watumishi wa afya na maji na usafi wa mazingira.

Aidha, AMREF inatekeleza miradi ya kijamii kwa kutoa elimu kwa watumishi, viongozi wa Dini na wahamasishaji kupitia vyombo vya habari kwa lengo la kudhibiti magonjwa ikiwemo UVIKO-19.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,263FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles