27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Chana akoshwa na mbio za magari shamba la miti Sao Hill

Na Raymond Minja, Mtanzania Digital

Waziri wa Maliasi na Utali, Balozi Dk. Pindi Chana ameipongeza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kupitia Shamba la miti Sao Hill kwa kutangaza utalii kupitia mashindano ya magari yaliyofanyika wilayani Mufindi mkoani Iringa.

Akizungumza kwa njia ya simu wa Kati wa kuhitimisha mashindano hayo Dk. Chana amesema Serekali imefurahishwa sana na mashindano hayo nakwamba iko tayari kuyaendeleza.

“Niwapongeze sana hapo Mufindi kwa ubunifu wenu, wsote tunajua kuwa hapo Mufindi kuna vivutio vingi, hivyo ni matarajio yetu mashindano hayo yataendelea na serekali chini ya mama yetu Rais Samia Suluhu Hassan tutaunga mkono juhudii zenu ili kuendeleza mashindano hayo na kukuza utalii wetu,” amesema Dk.Chana.

Amesema tangu Rais Samia azindue filamu ya The Royal Tour mwamko wa watali umekuwa mkubwa kwa kuongezeka kwa watali wengi nchini jambo ambalo linasaidia kukuza pato la taifa.

Saad Mtambule ni Mkuuu wa Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa ambapo amesema kuwa utalii wa mashindano ya mbio za magari ndani ya shamba la Sao Hill unakwenda kufungua fursa nyingi katika sekta ya utalii na wao wilaya wamejipanga kupokea wananchi na wawekezaji walio tayari kufanya uwekezaji ndani ya shamba hilo.

Amefafanua zaidi kuwa sekta hiyo imeendelea kukua kwa kasi kubwa kutokana na jitihada za Rais Samia tangu alipotangaza utalii kupitia filamu ya The Royal Tour.

“Tunamshukuru Mhe. Rais Samia kwa kuanzisha filamu ya Tanzania Royal Tour na sisi kupitia sekta ya misitu tumeona pamoja na kupata mbao na kutengeneza bidhaa mbalimbali zitokanazo na misitu tunaamini mashindano ya magari yataongeza fursa na kuleta bidhaa mpya kwenye sekta ya misitu.

“Pia tunawapongeza TFS kupitia shamba la miti Sao Hill pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii ikiongozwa na Balozi Dk. Pindi Chana kwa uratibu mzuri wa mashindano haya ya magari yanayofanyika hapa, kwetu mashindano haya yanakwenda kuongeza fursa nyingine kwa wananchi wetu,” amesema Mtambule.

Kwa upande wake Mhifadhi Mkuu wa shamba hilo, Lukas Sabida amesema mashindano hayo ya magari yamefanyika kwa mara ya kwanza ndani ya shamba hilo nakwamba yemefungua fursa za utalii mpya.

Kwa upande wao washiriki wa mashindano hayo, Ali Msigwa amepongeza uongozi wa shamba hilo kwa kubuni mchezo huo ndani ya misitu ya shamba hilo kwani awali walikuwa hawajui iwapo ndani ya misitu hiyo kunaweza kufanyika mashindano ya magari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles