32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Biteko: Uwepo wa SGR unaashiria utoshelevu wa umeme nchini

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk. Doto  Biteko amesema safari za treni za reli ya kisasa (SGR) zinazotumia umeme kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma ni ushahidi kuwa Tanzania ina umeme wa kutosha.

Dk. Biteko ameyasema hayo leo Septemba 12, 2024 baada ya kuwasili jijini  Dodoma akitokea Dar es Salaam kwa kutumia usafiri wa treni ya mwendo kasi (SGR) kwa mara ya kwanza.

“Safari za treni ya umeme ya SGR ni ushahidi mwingine kuwa nchi ya Tanzania ina umeme wa kutosha, ni ushahidi mwingine kwamba nishati ya umeme ikipatikana ya uhakika inafungua fursa mbalimbali za kiuchumi, viwanda mbalimbali vinajengwa na kongani za viwanda kuongezaka,”amesema Dk. Biteko

Ameongeza kuwa katika kuhakikisha umeme unatosheleza Wizara ya Nishati kazi yake ni kuhakikisha umeme unakuwepo wa kutosha wakati wote na  kuwa Wizara inasimamia ujenzi wa laini nyingine ya kuutoa umeme kutoka Chalinze hadi Dodoma kwa laini kubwa zaidi na kutoa umeme kutoka Bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere kwenda Dodoma baadae Singida, Arusha hadi Mwanza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles