Mwandishi wetu, Mwanza
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko amewataka wahitimu wa vyuo mbalimbali nchini kuchukia rushwa katika kuwahudumia wanachini.
Amesema baada ya kuajiriwa au kujiajiri wakasikilize na kuhudumia watu wa makundi yote hasa maskini kwani kila mwananchi ana haki ya kupata huduma bora bila kujali hadhi aliyonayo.
Amesema hayo leo Desemba 16,2023 katika Mahafali ya 26 ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino cha Tanzania (SAUT), yaliyofanyika katika Viwanja vya Raila Odinga jijini Mwanza.
“Ndugu Wahitimu na wale ambao tupo makazini, tusikilize watu wa makundi yote hasa wale wasio na kitu cha kutulipa na tuone fahari ya kunyanyua hadhi ya watanzania kwenda kwenye maisha yaliyo bora zaidi kwani ukisaidia maskini unakuwa umesaidia wananchi wengi zaidi,” amesema Dk.Biteko.
Amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri na wezeshi kwa kila mtu mwenye juhudi na kuhakikisha maeneo ya kufanya kazi yanakuwa bora, pia kuwezesha uwekezaji na kuajiri kwa wahitimu wa taaluma mbalimbali.
Katika hatua nyingine, Dk. Biteko amesema kuwa, Rais wa Dk. Samia Suluhu Hassan ametuma salam za pongezi kwa Jumuiya ya wana SAUT na wahitimu kwa mahafali hayo ya 26.
Amesema kuwa, Rais anaamini kwamba, uwepo wa Taasisi hiyo ya SAUT inaongeza mchango mkubwa katika mipango ya Serikali katika kusukuma mbele maendeleo ya nchi kupitia wahitimu wa kada mbalimbali katika