28.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 2, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Biteko ataka ulinzi miundombinu ya shule

Na Mwandishi Wetu

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko amewataka wazazi na walezi nchini kutumia fursa ya miundombinu ya shule inayojengwa kwa ushirikiano wa Serikali na wafadhili kuwasomesha watoto na hatimaye kuchochea maendeleo.

Dk. Biteko amesema hayo wakati akizindua miundombinu ya Shule ya Sekondari ya Milles and Kimbery White iliyojengwa kwa zaidi ya sh 12 bilioni wilayani Mkinga kwa lengo la kuwawezesha watoto wa eneo hilo kujikwamua katika ya elimu.

“Miundombinu imejengwa kwa gharama kubwa ni vema ikatunzwa na kuhifadhiwa ili iwe na manufaa kwa jamii na taifa kwa ujumla,” amesema.

Pia amewataka wanafunzi kutumia nafasi wanayoipata kujiendeleza kwa kujisomea na kujenga uelewa huku wakichukua tahadhari dhidi ya baadhi ya maudhui yanayopatikana katika mitandao ya kijamii kwa kufanya hivyo hawatajuta kutokana na matokeo mazuri watakayoyapata.

Kwa upande wake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolph Mkenda amesema Wizara yake imejipanga kuanzisha mafunzo ya amali ambapo shule zaidi ya 100 zitajengwa nchi nzima ili kuwawezesha wanafunzi wahitimu elimu wakiwa na ujuzi.

Amesema jitihada kubwa iliyotumika kuweka uwekezaji katika miundombinu ya shule hiyo italindwa na kuendelezwa ili kuhakikisha malengo yaliyokusudiwa.

Naye Mtendaji wa Mkuu wa ABBOTT, Robert Ford amesema ujenzi wa shule hiyo unakusudia kuwasaidia watoto katika eneo hilo kupata elimu na ujuzi huku akiwashukuru wakazi wa eneo la Mapatano kwa ushirikiano walionesha katika kipindi chote cha utekelezaji wa mradi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles