30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Biteko aitaka Jamii inayozunguKA migodi kuwa na uhusiano bora na Wawekezaji

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Madini, Dk. Doto Biteko amezitaka jamii zinazonguka maeneo ya migodi kutangaza mazuri yanayofanywa na wawekezaji katika Sekta ya Madini ili kuwatia moyo wa kufanya shughuli za madini.

Waziri wa Madini, Dk. Doto Biteko(aliyesimama) akizungumza.

Dk. Biteko ameyabainisha hayo, Julai 22, 2022 akiwa katika ziara yake kijiji cha Kagerankanda wilaya ya Kasulu alipotembelea mgodi wa Kampuni ya Life Business unaochimba madini ya Chokaa mkoani Kigoma.

Amesema, migogoro baina ya wawekezaji katika Sekta ya Madini na wananchi katika maeneo mengi ya migodi imewafanya wawekezaji kupata hofu ya kuwekeza katika uchimbaji wa madini katika baadhi ya maeneo na hivyo kupunguza uzalishaji.

Amewataka wananchi kuhakikisha wanajenga mahusiano mazuri na wawekezaji ili kutatua changamoto zinazojitokeza kati yao ili wawekezaji waweze kutekeleza huduma mbalimbali za kijamii katika maeneo yanayozunguka migodi.

Aidha, Dk. Biteko ameahidi kuwa, changamoto zilizopo za ukosefu wa barabara na ujenzi wa madarasa zitafanyiwa kazi haraka baada ya kutoa maelekezo kwa mwekezaji huyo.

Kwa upande wake, mmiliki wa mgodi huo ndugu Lister Balegele ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la vyama vya wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA) amesema, Kampuni hiyo imekuwa ikilipa mapato ya Serikali na michango mbalimbali kutokana na mauzo ya madini ya chokaa.

Kuhusu huduma za kijamii Balegele amesema, mgodi unajenga madarasa mawili mpaka sasa katika shule ya sekondari hapo kijijini, wametoa madawati 50 kwa ajili ya shule pamoja na kugawa kompyuta mpya kwa shule ya sekondari na msingi.

Baada ya ziara ya Dk. Biteko katika mgodi huo, mwekezaji wa mgodi huo ameahidi kukamilisha barabara na ujenzi wa madarasa hivi karibuni.

Naye, Mjiolojia Mwandamizi kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) John Kalimenze amesema, Serikali kupitia taasisi hiyo itaendelea kufanya tafiti za madini ili iweze kugundua maeneo zaidi kwa ajili ya uchimbaji na kuongeza tija kwa wachimbaji na kuongeza mapato ya Serikali.

Aidha, amemuhakikishia mwekezaji kupata ushirikiano wa kitaalamu toka GST katika kuendeleza mgodi wake kwa kutambua ubora na wingi wa mashapo ya malighafi ya mawe ya chokaa yaliyopo katika leseni au eneo lake.

Mgodi huo kwa sasa unachimba madini ya chokaa na kusafirisha yakiwa ghafi na kuuza katika kiwanda cha Burundi Cement Company (BUCECO) kupitia mpaka wa Manyovu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles