24.9 C
Dar es Salaam
Sunday, April 21, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Bilal: Dawa za kulenya hatari kwa Taifa

NA ELIUD NGONDO, MBEYA

MAKAMU wa Rais,

Dk. Mohammed Gharib Bilal
makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal

, amesema wimbi la uingizwaji wa dawa za kulevya nchini limekuwa tishio kwa Taifa.

Amesema hali hiyo imekuwa ikiharibu nguvu kazi, kuzorotesha afya za watumiaji na hata kuongeza vitendo vya uhalifu katika jamii.

Hayo aliyasema jijini Mbeya jana alipokuwa akihutubia katika kilele cha maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupiga vita Dawa za Kulevya Duniani, ambapo alisema matumizi ya dawa hizo yamekuwa yakichochea ongezeko la maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi nchini.

Dk. Bilal alisema hali hiyo imekuwa ikichochea kufanyika kwa ngono zembe kwa watumiaji pamoja na kuchangia sindano za kujidungia hali inayohatarisha usalama wao na Taifa kwa ujumla.

“Madhara mengine wanayoyapata watumiaji ni maradhi mbalimbali kama homa ya ini, mapafu, moyo na Kifua Kikuu hali hii ni hatari kwa nguvu kazi za vijana na kwa Taifa letu.

“Inasikitisha sana kwamba vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa wamekuwa wakijihusisha na biashara ya dawa hizi nje ya nchi na takwimu za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuanzia mwaka 2006 hadi 2013 Watanzania 178  wanatumikia kifungo nchini China,” alisema Dk. Bilal.

Alisema hadi kufikia Aprili mwaka huu Watanzania 113 ambao walifungwa nchini Brazil kwa kujihusisha na biashara hiyo jambo linaloleta taswira mbaya kwa nchi kimataifa kwa kuonekana ni wazalishaji wakubwa wa dawa hizo.

“Kuanzia Januari 2009 hadi 2014, Jeshi la Polisi limewakamata watuhumiwa 13,846 wakijihusisha na biashara za dawa za kulevya hapa nchini na kilo 966.06 za Heroni, kilo 363.7 za Cocaine, kilo 45,734 za mirungi tani 212.071 za bangi zilikamatwa,” alisema.

Alisema changamoto kubwa iliyopo hivi sasa duniani ni kudhibiti dawa za kulevya na kuibuka kwa dawa mpya za kulevya ambazo udhibiti wake ni lazima ihusishe mikataba ya kimataifa.

Dk. Bilal, alisema kaulimbiu ya mwaka huu ni ‘Uteja wa Dawa za Kulevya Unazuilika na Kutibika’ chukua hatua ikiwa na maana ya kuepuka matumizi ya dawa za kulevya ili kujenga jamii yenye afya njema, uchumi imara na yenye usalama.

Akitoa takwimu za mwaka 2011 hadi 2014, alisema watumiaji wa dawa hizo za kulevya 1,526 walikuwa wakiendelea kutumia dawa aina ya Methadone katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kuwa wanawake ni 205 huku wanaume ni 1,321.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles