25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Abbas akabidhi Idara ya Habari, ajivunia mafanikio

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

KATIBU Mkuu Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk.Hassan Abbas ameikabidhi rasmi Idara  ya Habari kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Zainabu Chaula huku akidai anaamini amekabidhi kwenye mikono salama.

Hatua hiyo imekuja kufuatia hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kufanya mabadiliko kwa kuihamisha idara ya Habari  kwenda Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Oktoba 18,2021,wakati wa makabidhiano hayo,Katibu Mkuu huyo amesema mabadiliko hayo yamelenga kuongeza zaidi nguvu kwenye sekta ya wizara hizo mbili huku akiweka bayana kuwa anaiacha Ofisi hiyo  ikiwa na wafanyakazi 37 na vifaa mbalimbali muhimu kwa ajili ya utekelezaji majukumu.

“Nasikia huzuni kuondoka, nilizoea, naondoka nikiamini ufanisi utaongezeka, wakati naanza hakukuwa na gari lakini sasa naondoka nikiwa naacha magari manne, kitengo hiki kina Ofisi mbili Dar es Salaam na Dodoma,”amesema.

Dk.Abbas ameeza kuwa sekta ya habari ina mafanikio makubwa ambapo kwa sasa ina magazeti yaliyosajiliwa  270 ,Televisheni  51,Radio 298, Televisheni mtandao 496 na Radio mtandao 500.

“Namkabidhi idara ya hii nikiwa na matumaini kuwa  maboresho zaidi yatafanywa  kuleta jita,”ameeleza Dk.Abbas.

Aidha ameeleza mafanikio yaliyopatikana kwenye sekta hiyo kuwa ni pamoja na  yamepatikana kutokana na kanuni sita walizojiwekea ambazo ni kuweka mipango mikubwa, kutekeleza mipango yote,kufanya kazi kwa ushirikiano, mawasiliano ya pamoja katika  kutatua kero na kumuachia mwenyezi mungu yale yaliyo nje ya uwezo wao.

“Mafanikio yote yaliyopo yamepatikana kutokana  na kanuni hizi sita,tuliamini kuwa hakuna linalowezekana bila ushirikiano,” amesisitiza.

Pamoja na mambo mengine, Dk.Abbas ametumia nafasi hiyo kutoa wosia kwa tasnia ya Habari kwa kuwataka Waandishi wa Habari kuwa na wivu na taaluma yao ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa zenye usahihi,ukweli na umakini.

Kwa upande wake Dk. Chaula ameeleza kuwa Dkt.Abbas anaondoka akiwa ameacha  mchango mkubwa katika idara hiyo.

“Natambua utumishi wetu uzae matunda zaidi,naelewa tunafanya kazi na kupitia changamito nyingi,naahidi  nitafanya kwa kufuata kanuni zote hizo sita kwa maendeleo ya Wizara yangu,” amesema.

Mbali na hayo amewata Wafanyakazi hao 37 wa Wizara hiyo kumpa ushirikiano na kufanya kazi kwa uadilifu na matokeo makubwa.

“Nakupongeza sana Dk.Abbas na timu yako ,tunaingia na naahidi nitaboresha ulipoacha,changamoto zilizopo mimi kwa kushirikiana  na wenzangu tutazifanyia kazi lakini pia mafanikio yaliyopo tunayaendeleza,”amesema Chaula.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles