27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Dimpoz: Sitamtangaza mpenzi wangu kama maonyesho

Ommy-DimpozNA JENNIFER ULLEMBO
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, amesema hataki kuweka wazi uhusiano wake wa kimapenzi na mpenzi wake kama wafanyavyo baadhi ya wasanii ndani na nje ya Tanzania.
Dimpoz alisema watakaomfahamu mpenzi wake ni watu wake wa karibu na si kila shabiki wake kwa kuwa mambo ya mapenzi yanapendeza yakiwa siri.
“Hakuna haja ya kufanya maonyesho ya mapenzi kwa mashabiki, uhusiano wangu ni mimi na mpenzi wangu, hakuna haja ya kila mtu kujua kwa sababu mapenzi si maonyesho,” alieleza msanii huyo.
Dimpoz alimaliza kwa kudai kwamba maisha yake binafsi yataendelea kuwa binafsi na muziki wake ndiyo utakuwa kwa mashabiki zake wote kwa kuwa unawahusu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles