27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Diamond Platnumz kivutio kwa watalii Gombe

Nasib Abdul ‘Diamond’
Nasib Abdul ‘Diamond’

NA NORA DAMIAN, KIGOMA

WATALII wengi katika Hifadhi ya Taifa ya Gombe iliyoko mkoani Kigoma, wamevutiwa na vipande vya video ya wimbo wa Leka Dutigite’ ulioimbwa na wasanii wanaotokea Mkoa wa Kigoma ‘Kigoma All Stars’, kutokana na kutumia mazingira ya hifadhi hiyo.

Kipande kinachouliziwa zaidi na watalii wanaofika katika hifadhi hiyo ni kile kinachomwonyesha mkali wa muziki wa Bongo Fleva, Nasib Abdul ‘Diamond’ akiwa anabembea katika mti ulioko katika hifadhi hiyo.

Mhamasishaji Utalii Msaidizi katika hifadhi hiyo, Isaya Mkude, alisema watu wengi hasa wazawa wamekuwa wakifika na kutaka waonyeshwe sehemu alipobembea msanii huyo.

“Tumeamua kuiita bembea ya Diamond kwa sababu baada ya yeye kubembea imekuwa kivutio kwa watu wengi kuja na kutaka kwenda kupaona na wengine kubembea,” alisema Mkude.

Alisema miaka ya nyuma wageni ndio walikuwa wengi wanaotembelea hifadhi hiyo lakini hivi sasa kuna mwamko mkubwa kwa wazawa.

Takwimu za mwaka 2014/15 zinaonyesha wazawa waliotembelea hifadhi hiyo ni 527 wakati wageni ni 927. Kwa mwaka 2015/Mei 2016 wazawa ni 374 na wageni ni 645.

Gharama ya kuingia katika hifadhi hiyo ambayo ni maarufu kwa wanyama aina ya sokwe ni Sh 10,000 kwa Mtanzania mmoja na Dola 100 kwa mgeni kwa siku.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles