22.9 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Black Coffee wa BET kufanya kazi na Alicia Keys

 Black Coffee
Black Coffee

NEW YORK, MAREKANI

MSHINDI wa tuzo ya Black Entertainment Television (BET), barani Afrika, Nathi Maphumulo maarufu kwa jina la Black Coffee, amepata dili la kufanya kazi na msanii wa Marekani, Alicia Keys.

Wawili hao wanatarajia kufanya wimbo wa pamoja baada ya mume wa Alicia, Swezz Beats, kufuatilia kazi za msanii huyo kutoka nchini Afrika Kusini na kumshauri mke wake afanye naye kazi hivi karibuni.

Hata hivyo, Black Coffee, amedai kwamba tuzo hiyo ya BET itazidi kumpa mafanikio makubwa ndani na nje ya nchi.

“Wengi walikuwa hawajui uwezo wangu, lakini ninaamini baada ya kupata tuzo hiyo nitazidi kufahamika zaidi, kuna jambo kubwa ambalo linatarajia kutokea hivi karibuni, kuna mazungumzo yanaendelea na Alicia Keys ila siliweki wazi kwa sasa hadi pale mambo yatakapokamilika, lakini watarajie jambo kubwa,” alieleza Black Coffee.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles