31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

DHAMANA YA LEMA YAENDELEA KUKWAMA

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), akipunga mkono jana nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, wakati akirudishwa katika mahabusu ya gereza kuu la Kisongo baada ya mahakama kushindwa kutoa uamuzi wa hatima ya dhamana yake.
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), akipunga mkono jana nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, wakati akirudishwa katika mahabusu ya gereza kuu la Kisongo baada ya mahakama kushindwa kutoa uamuzi wa hatima ya dhamana yake.

Na JANETH MUSHI – ARUSHA


 

DHAMANA ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), imeendelea kuwa kitendawili baada ya mawakili wa Serikali kukata rufaa Mahakama ya Rufaa Tanzania, kupinga Jaji Salma Magimbi kusikiliza rufaa yao wenyewe.

Jaji Magimbi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha, jana alikuwa atoe uamuzi juu ya rufaa iliyowasilishwa na upande wa Jamhuri kupinga Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kumpa dhamana Lema.

Akiahirisha uamuzi huo jana mahakamani hapo, jaji huyo alisema hawezi kusikiliza na kutoa uamuzi kwa kuwa mawakili wa Serikali walisajili nia ya kusudio la kukata rufaa Desemba 30, mwaka jana, katika Mahakama ya Rufaa Tanzania iliyopo mkoani hapa, kupinga asisikilize rufaa hiyo.

Desemba 28, mwaka jana, mahakama hiyo ilipanga kusikiliza rufaa ya maombi ya dhamana ya Lema namba 126 ya mwaka 2016.

Lakini kutokana na mawakili wa Serikali kukata rufaa hiyo, mawakili wa mlalamikiwa walisema ni vema mahakama hiyo ikaanza kusikiliza kwanza rufaa ya Jamhuri kwa vile kinachobishaniwa ni dhamana ya Lema.

Jaji Magimbi aliyekuwa anasikiliza rufaa hiyo, aliwataka mawakili wa Jamhuri kuwasilisha hoja zao za rufaa Desemba 29, mwaka jana huku mawakili wa Lema wakitakiwa kujibu hoja hizo Desemba 30, kabla ya mahakama haijatoa uamuzi wa rufaa hiyo jana.

Katika shauri hilo, upande wa Jamhuri unawakilishwa na Wakili Innocent Njau na Lema anatetewa na jopo la mawakili watano wakiongozwa na Peter Kibatala. Mawakili wengine ni John Mallya, Adam Jabir, Sheck Mfinanga, Charles Adiel na Faraji Mangula.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles