26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

DEFOE KUMUENZI BRADLEY LOWERY

LONDON, ENGLAND

MSHAMBULIAJI mpya wa klabu ya Bournemouth na timu ya Taifa ya England, Jermain Defoe, anatarajia kumuenzi marehemu Bradley Lowery katika mchezo wa watu maarufu wa kuchangia mfuko wake, Septemba 3 kwenye uwanja wa Goodison Park.

Lowery ambaye alikuwa ni shabiki mkubwa wa klabu ya Sunderland, alipoteza maisha Julai mwaka huu baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani kwa kipindi kirefu, hivyo baadhi ya watu maarufu wanatarajia kucheza mechi kwa ajili ya kupata fedha za kuuendeleza mfuko wa shabiki huyo.

Defoe alikuwa mmoja wa rafiki wa karibu na Lowery tangu akiwa katika kikosi cha Sunderland, hivyo ameweka wazi kuwa yupo tayari kucheza mchezo huo kwa ajili ya kumuenzi rafiki yake kipenzi.

“Nipo tayari kushiriki mchezo huo wa kuchangia mfuko wa marehemu Bradley Lowery, ninaamini mchezo huo utakuwa muhimu sana kwangu, hata kama sitapata nafasi ya kucheza lakini lazima niwe uwanjani kuuangalia.

“Nitafanya hivyo kwa kuwa Bradley alikuwa rafiki yangu wa karibu sana na bado nipo karibu na familia yake. Napenda kuchukua nafasi hii kuishukuru Everton kwa niaba ya familia ya Bradley pamoja na familia yangu kwa kile walichokifanya hadi kufanikisha suala hilo.

“Pia napenda kutumia nafasi hii kuwashukuru wale wote walioanzisha suala hilo, ninaamini tutafanikiwa kupata kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya mfuko huo wa familia ya Bradley Lowery,” alisema Defoe.

Mastaa hao watatengeneza timu mbili ambazo zitaitwa Bradley Blue ikishabikiwa na familia ya Bradley, wakati huo timu nyingine itajulikana kwa jina la Lowery Legends.

Bingwa wa ngumi nchini Uingereza, Tony Bellew, atakuwa kocha wa timu ya Bradley Blues, huku ikiwa na wachezaji kama vile Olly Murs, Stephen Graham, Shayne Ward na wachezaji wa zamani wa Everton, Peter Beardsley na Alan Stubbs.

Kwa upande wa timu ya Lowery Legends, itakuwa chini ya mkongwe wa zamani wa timu ya Liverpool, Roy Evans na mwanamitindo nchini Uingereza, Katie Price, huku timu yao ikiwa na wachezaji kama vile Calum Best, Jeremy Lynch, Josh Cuthbert, Alex Rae na Don Hutchison.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles