25.3 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

DED Muleba awasihi wanafunzi kuzingatia masomo

Renatha Kipaka, Muleba

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, Elias Kayandabila ametembelea shule za Sekondari ya Kaigara, Anna Tibaijuka, Kasharunga na Shule ya Sekondari ya Kasharunga Mpya (Kiteme) kukagua mwitikio wa wanafunzi wa kidato cha kwanza huku akiwasihi wanafunzi hao kuzingatia watayofundishwa.

Wito huo ameutoa mapema wiki hii alipotembelea shule hizo ambapo amewasihi wanafunzi hao kutunza miundombinu ya madarasa huku akiwaeleza kuwa wamepata nafasi ya kusomea katika mazingira yaliyo bora hivyo anatarajia watafanya vizuri na hatimaye kuwa na ufaulu mzuri.

“Nitumie Fursa hii kuwaambia kuwa Nimefurahi mnoo kusikia mnafahamu madarasa yamejengwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, fadhila pekee ambayo tunaweza kumlipa mama ni kufanya vizuri kwenye masomo yenu nakuhakikisha mnafauru kwa kishindo,” amesema Kayandabila.

Hata hivyo, akiwa shule mpya ya Kasharunga amewasihi wazazi na jamii kuisaidia Serikali kuwabaini watoto ambao wamefaulu lakini watoto au wazazi wao wamelazimisha kwenda kuolewa ili serikali iweze kuchukua hatua dhidi yao na kuwarudisha shule watoto hao kwani malengo ya serikali ni watoto wote waliofaulu waendelee na masomo.

Afisa Elimu Sekondari wa wilaya ya Muleba. Masatu Chisumo amewasihi wanafunzi kutunza vyumba vya madarasa na kuwataka walimu kuanza ratiba za vipindi.

Mkuu wa Shule ya Anna Tibaijuka mwalimu Paulo Mligo ametoa shukrani kwa Rais Samia kwa kutoa fedha za ujenzi wa vyumba vya madarasa mapya vya kisasa ambavyo vimesaidia kupunguza uhaba na kuahidi kwamba watavitunza vyumba hivyo vya madarasa ili viweze kuwasaidia na wanafunzi wengine kwa miaka ijayo.

Kwa upande wake mwanafunzi wa kidato cha kwanza shule ya Sekondari Anna Tibaijuka kwa niaba ya wanafunzi wenzake ametoa shukrani na pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa vya kisasa na kuahidi kuwa atasoma kwa bidii ili kuweza kufikia ndoto zake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles