25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

DC Nguvila amtaka mkandarasi wa barabara ya Kimeya kuongeza kasi

Na Renatha Kipaka, Muleba

Mkuu wa Wilaya ya Muleba mkoani Kagera, Toba Nguvila amemtaka Mkandarasi wa ambayeni kampuni ya DRK ya Karagwe, anayejengeza barabara ya Kimeya-Burigi kuongeza kasi ya matengenezo na kukamilisha kazi aliyopewa kwa wakati kama ambavyo mkataba wake unaeleza.

Mkuu wa Wilaya ya Muleba mkoani Kagera, Toba Nguvila.

Nguvila ametoa agizo hilo jana baada ya kukagua ujenzi wa barabara zinazohudumiwa na TARURA zilizo katika hatua mbalimbali za matengenezo.

Amemtaka Mkandarasi huyo kuhakikisha anafanya kazi kwa bidii ili aweze kutimiza malengo ya kimkataba pamoja na kuimarisha huduma ya usafiri na mawasiliano kwa wananchi wa Muleba hususan wa maeneo ya Kimeya hadi Burigi.

“Nimefika kukagua, nimejionea kazi mnayofanya. Hivyo, nimefurahishwa na kasi nzuri mnayoendelea nayo maana barabara hii ilichelewa kuanza kutokana na matatizo ya Mkandarasi aliyepewa kazi awali. Nataka mfanye kazi kwa kasi na kuimaliza ndani ya wiki mbili sitaki stori,” amesema Nguvila.

Aidha, amemsisitiza mkandarasi kuhakikisha anamaliza kazi kwa wakati ili kuweza kusaidia usafirishaji wa vifaa vya ujenzi vitakavyotumika katika ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Karambi inayojengwa katika eneo la kijiji Itunzi, kata ya Karambi.

Wakati huo huo ametoa rai kwa mkandarasi kuhakikisha vifaa vya matengenezo vinakuwepo vya kutosha na kusisitiza kuwa atakwenda kukagua tena maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo ili kujiridhisha kama ametekeleza kwa ubora.

Kwa upande wake Mhandisi msimamizi wa DRK Company, Jonston Kajwahula ameeleza kuwa wameanza na matengenezo ya sehemu korofi, mhandisi alifika na kuwapa maelekezo kwenye eneo la tingatinga kujaza kifusi, tayari wamefuata greda lingine kwa ajili ya kuongeza nguvu na kumaliza barabara hiyo kabla ya mvua hazijaanza kunyesha.

Kwa upande wake Meneja wa TARURA wilaya ya Muleba, Mhandisi Dativa Telesphory amesema kuwa kazi zitakazofanyika katika barabara hiyo ni uchongaji wa barabara Km 18.5 na kuweka kifusi cha moramu km 5.8 na kazi nyingine ni kuhakikisha anaondoa udongo ambao austahili ndani ya barabara, kuchimba mitaro na kutoa maji kwenye barabara kwa gharama ya Sh milioni 103.5 ambapo mpaka sasa amefikia asilimia 35 ya ujenzi wa barabara hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles