27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

DC Muleba ataka walimu watiwe moyo kwa kupewa Viwanja

Na Renatha Kipaka, Bukoba

Mkuu wa Wilaya ya Muleba mkoani Kagera, Toba Nguvila amesema ili kuwatia moyo walimu na kuendelea kujituma wapewe zawadi ya Viwanja ili iwe kumbukumbu kwao.

Nguvila ametoa kauli hiyo juzi katika kikao cha kamati ya ushauri cha Mkoa (RCC) na nakwamba kufanya hivyo nikuwatia moyo walimu ili waendelee kufundisha kwa bidii na kuongeza ufaulu mkubwa kwa wanafunzi mkoani humo.

Hata hivyo, amesema utaratibu wa kuwapa walimu zawadi ya fedha hausaidii sana katika kuongeza nguvu ya kufundisha.

“Nitumie fursa hii kusema kuwa ili kutoa motisha kwa walimu wetu kila halmashari itenge eneo ambalo litatumika kuwapa walimu zawadi kulingana na jitihada zao.

“Unaangalia ni nani aliyefaulisha vizuri kwa madarasa mfano darasa la saba, kidato cha nne na sita, mwalimu anapewa kiwanja kimoja au vitatu,” amesema Nguvila.

Naye Afisa Elimu wa Mkoa wa Kagera, Alphan Semaonge amesema hali ya taaluma kwa mkoa katika darasa la nne, la saba na kidato cha pili nne na sita inaridhisha.

Amesema mwaka 2019 ufaulu wa darasa la nne ulikuwa asilimia 97.9 ambapo 2020 ulishuka kwa asilimia 2 hadi kufikia 95

Semaonge amesema kwa kidato cha pili na nne ufaulu uliongezeka kwa asilimia 0.2 kwa mwaka 2020 ikilinganishwa na 2019 kuwa na asilimia 83 hadi kufikia asilimia 88 sawa na ongezeko la asilimia 2.3

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles