24 C
Dar es Salaam
Thursday, July 25, 2024

Contact us: [email protected]

DC Korogwe amzawadia 300,000 Mkuu wa Shule iliyokamilisha madarasa

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, Basilla Mwanukuzi ametoa zawadi ya Sh 300,000 kwa Mkuu wa shule ya Sekondari Mbaghai, Sadiki Dilunga ambaye shule yake ilikuwa ya kwanza kukamilisha madarasa ndani ya wilaya hiyo tangu Novemba 19, mwaka huu.

Mwanukuzi ametoa zawadi hiyo leo Jumamosi Desemba 17, 2022 kama pongezi kwa mkuu huyo wa shule sambamba na kutambua mchango wa kila mmoja katika kusukuma maendeleo ya elimu wilayani humo.

“Kwa namna ya pekee ninampongeza Mkuu wa Shule kwa niaba yetu, sote kwa kazi kubwa na nzuri ya kutii maagizo ya Serikali na kuwa wa kwanza kukamilisha ujenzi.

“Niliahidi na leo nimetimiza baada ya kukagua ujenzi na kuridhika na kazi kwa kusimamiwa na Mkuu wa Shule, ukale sikukuu na familia. Nitaendelea kutambua mchango wa kila mmoja wetu na kila mtumishi katika kila ngazi na kila sekta na kupeana moyo katika kulitumikia taifa letu hususan wilayani Korogwe,” amesema Mwanukuzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles