25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

DC Kigamboni aipa tano UBA Tanzania kutoa msaada wa vitabu

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri, ameipongeza Benki ya UBA Tanzania kwa mchango mkubwa inaotoa kwenye sekta ya elimu hususani kutoa vitabu zaidi ya 15,000 kwa shule za sekondari zote zenye uhitaji wa vitabu zilizopo wilaya humo.

UBA Tanzania kupitia UBA Foundation chini ya mpango wa ‘Read Africa Initiative’, imetoa vitabu hivyo vya fasihi kwenye shule za sekondari za serikali zilizopo Wilaya Mpya ya Kigamboni katika shule za Nguva, Aboud Jumbe na Pemba Mnazi.

“Vitabu hivi vilivyotolewa na Benki ya UBA Tanzania, vitasaidia katika kuwajengea vijana wetu kupenda kujisomea na kujiwekea utaratibu wa kujisomea mara kwa mara, pamoja na kuwaongezea uwezo katika masomo yao,” amesema Msafiri.

Baadhi ya wanafunzi wa Shule za Sekondari wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam, wakifurahia vitabu walivyopatiwa na Benki ya UBA Tanzania.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Biashara Ndogo Ndogo na Kati, Geofrey Mtawa, amesema vitabu hivyo ni vya hadhi ya juu Afrika, ambavyo vimeboreshwa zaidi ili kuwawezesha wanafunzi na walimu kuvielewa kwa lugha rahisi na yenye kuelimisha.

Baadhi ya vitabu vilivyotolewa na benki hiyo ni vile vinavyotumika kwenye mitaala ya Tanzania kama ‘Things Fall Apart’, ‘The Girl That Can’, ‘The Fisherman’ na vinginevyo.

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya UBA Tanzania, wakifurahi na wanafunzi wa Shule za Sekondari za Wilaya ya Kigamboni ambazo benki hiyo imetoa msaada wa vitabu.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles