30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, March 26, 2023

Contact us: [email protected]

RC Mtwara aahidi ushirikiano na wawekezaji kwenye korosho

Florence Sanawa, Mtwara

Mkuu waMkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa amesema atawapa ushirikiano wawekezaji kwenye sekta mbalimbali mkoani humo ikiwamo zao la korosho.

Akizungumza wakati wa kongamano la siku mbili la uwekezaji la kimataifa la korosho lililoandaliwa na Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) mjini Mtwara ambalo limekutanisha wawekezaji 73 wa viwanda kutoka mataifa  zaidi ya 20.

“Mwekezaji yeyote atakayehitaji eneo la kufanyia uwekezaji wowote wa hoteli na viwanda vya ubanguaji wa korosho atapewa ushirikiano mkubwa na hakutakuwa na urasimu wowote tuko tayari maeneo yametengwa na tunaamini kuwa uwekezaji huo utakuwa na tija kubwa kwa nchi,” amesema Byakanwa

Naye Mwenyekiti wa Bodi wa TIC, Longinus Rutasitara amesema, kongamano hilo limetoa mwanga mkubwa kwa wawekezaji hao ambapo kutafanyika utaratibu kwa mikoa mingine kwenye zao yale ya kimkakati kama vile kahawa, mahindi na mengine ili kuangalia namna bora ya kuyapatia thamani mazao hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,184FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles