28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

DC Iramba apiga marufuku wanunuzi wa mazao ya kilimo shambani

Na Seif Takaza, Iramba

MKUU wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman Mwenda amepiga marufuku wanunuzi wa mazao ya Kilimo kutoka nje ya nchi kununua mazao hayo yakiwa shambani.

Agizo hilo limetolewa juzi na Mkuu huyo wa Wilaya wakati akifungua kikao cha kuwajengea uelewa wafanyabiashara wa mazao ya kilimo Wilayani Iramba kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mjini Kiomboi.

Amesema ni jukumu la Serikali kutoa miongozo mbalimbali hususan urasimishaji wa mazao ya kilimo ili jamii na wafanyabiashara kuelewa utaratibu unaosimiwa Wizara ya Kilimo ambapo Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) na mamlaka nyingine unaratibu ili kuwalinda wakulima na wafanyabiashara dhidi ya usumbufu na utapeli unaotokea katika biashara ya mazao ya kilimo.

“Ndugu wafanyabiashara wa mazao ya kilimo, Serikali yenu inataka kuwajengea mazingira mazuri ya kufanya biashara ya mazao ya kilimo, haiwezekani mfanyabiashara kutoka nje ya nchi kuja kununua mazao yote yaliko shambani hivyo natamka kuanzia sasa ni marufuku kwa mfanyabiashara au mnunuzi kutoka nje ya nchi kununua mazao yakiwa shambani,” amesema Mwenda.

Aidha, Mkuu huyo wa wilaya alisema Serikali inakusudia kuwalinda wakulima na wafanya biashara hivyo kurasimisha sekta ya kilimo kwa kufanya biashara ya mazao ya kilimo kwa mujibu wa sheria.

Kwa upande wake, Fikiri Katiko, ambaye ni mchumi kutoka wizara ya kilimo lengo la wizara ya kilimo ni kuwasaidia wakulima wa Tanzania kunufaika kutokana na jitihada za Serikali za kutoa ruzuku na uwekezaji unaoendelea ili kupunguza gharama za kilimo na kuongeza uzalishaji na kuwezesha upatikanaji wa taarifa sahihi za biashara ya mazao ya kilimo.

“Mheshimiwa mkuu wa wilaya katika mukhtadha huu kila halmshauri itaainisha na kutangaza vituo vya ununuzi na uuzaji wa mazao ya kilimo ambapo vitu hivyo ni lazima viwe na mizani ya kupimia mazao iliyothibitishwa ubora na wakala wa vipimo, vituo hivyo viwe karibu na wakulima na vinavofikika kwa urahisi ili kuondoa usumbufu kwa wakulima,” amesema Katiko.

Amesema wafanya biashara wote wa mazao ya kilimo wanapaswa kusajiliwa mkoani au halmashauri husika na wanapaswa kulipa ushuru wote unaotakiwa kulipwa kwa mujibu wa sharia na wafanyabiashara kutoka nje ya nchi wanapaswa kupata kibali cha kusafirisha mazao ya kilimona kutoka wizara ya kilimo.

“Wanunuzi wa mazao kutoka nje ya nchi watalazimika kununua mazao kupitia kwa wafanyabiashara wa mazo ya kilimo waliosajiliwa na siyo kununua mashambani, lakini pia wafanyabiashara/ wanunuzi hao wanatakiwa kuwa na nyaraka zote muhimu ikiwemo utambulisho wa namba ya mlipa kodi yaani TIN, Leseni ya biashara ya kusafirisha nje ya nchina nyaraka nyingine muhimu zinazokidhi usafirishaji mazao nje ya nchi,” amesema Katiko.

Naye, Afisa Kilimo na Mifugo na Ushirika, Mareitha Kasongo amesema ni jukumu la wafanyabisahara na wanunuzi wa mazao ya kilimo kufuata sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya nchi katika kufanyabiashara ya mazao ya kilimo ni marufuku kutumia madalali wakati wakuomba vibali vya kusafirisha mazao ya kilimo nje ya nchi bali waombe moja kwa moja kupitia mfumo wa ATMIS au kufika katika ofisi za Wizara ya Kilimo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles