27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

DC Iramba aipa tano NMB, vijana waaswa

Na Seif Takaza,Singida

MKUU wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman Mwenda ameipongeza Benki ya NMB Tawi la Kiomboi kwa kufuturisha kwani kwa kufanya hivyo ni kumpendeza Mwenyeezi Mungu na Mtume Muhammad SAW.

Mwenda ametoa pongezi hizo juzi katika hafla ya futari ilioandaliwa na Benki hiyo katika Ukumbi Mkubwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mjini Kiomboi. 

Mwenda amesema Meneja wa Benki wa Tawi la Kiomboi, Juma Sololoka na Wafanyakazi wenzake wamefanya jambo zuri lakumpendeza Mwenyeezi Mungu na Mtume ambapo katika biashara yao wameona katika faida yao wanayopata wampe Mwenyeezi Mungu.

“Mimi Mkuu wa Wilaya hii nakupongeza sana, Juma Sololoka pamoja na wenzako kubuni  njia hii ambayo imewaunganisha Waislaam pamoja na wateja wako wa Benki na jamii  hivyo Mwenyezi Mungu awabariki, kitendo hiki kimeonyesha umoja na mshikamano wa pamoja lakini pia natoa wito kwa Taasisi zingine kuiga mfano wa NMB,” alisema Mwenda.

Kwa upande wake Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Kiomboi, Juma Sololoka alisema kuwa anamshukuru Mkuu wa Wilaya, Suleiman Mwenda, Alhaj Sheikh Omar Hassan Rukumbwe ambaye ni mjumbe wa Baraza la Masheikh Mkoa wa Singida na Imam Mkuu wa Msikiti wa Taqwa Mjini Kiomboi, Waumini wa Dini ya Kiislaam na waalikwa wateja wa benki hiyo kkwa kuhudhuria tukio hilo.

“Kwa heshima na taadhima na kwa uwezo wa Allah Subhanah Wataallah na baraka za Mtume wetu Muhammad SAW nawashukuru ninyi nyote mlioshiriki futari tuliyoiandaa kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani hasa kumi hili la mwisho huwa tunafuturisha ,Benki yetu imeona umuhimu kutumia faida tunayoipata katika benki yetu  tumpe na Mwenyeezi Mungu ili atupe baraka zake ili benki yetu iweze kufanya kazi kwa tija na ufanisi,” alisema Meneja Sololoka.

Naye Mjumbe wa Baraza la Msheikh Mkoa wa Singida na Imam wa Msikiti wa Taqwa, Alhaj Omar Hassan Rukumwe aliishukuru NMB kwa kufuturisha kwani kwa kufanya hivyo amefuata maagizo ya Quran na Sunnah kuhusu kutumia mali iliyochumwa kwa ajili ya kutoa sadaka kwa Waislam na jamii kwa ujumla.

Alhaj Rukumbwe alitoa wito kwa viongozi wa dini, wazazi na jamii kwa ujumla kuwaelekeza watoto na vijana kufuata maadili mema na mila na desturi zetu.

“Kwa sasa limejitokeza wimbi la vijana wetu kufuata maadili ya kigeni ukiwemo ushoga na usagaji vitendo ambavyo havilingani na maadili yetu, pamoja na maamrisho ya dini zetu hivyo natoa wito  kwa jamiii yote kukemea kwa vitendo. Inatubidi viongozi wa dini wazazi na jamiii kwa ujumla jambo hili tusilipe nafasi katika Wilaya yetu na Taifa ujumla vile sasa hivi kuna mambo mabaya ya udhalilishaji vya  ulawiti  wa Watoto na unyanyasaji wa kijinsia na vitendo hi tusivipe nafasi pia,” alitilia mkazo Alhaj Rukumbwe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles