27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

DC Bariadi: Bodi ya Pamba inakwamisha uchumi wa viwanda

Derick Milton, Simiyu

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga, amesema kama kuna mtu ambaye atafanya Tanzania isiwe nchi ya viwanda ni Bodi ya Pamba nchini.

Amesema bodi hiyo haina hata takwimu za mahitaji halisi ya mbegu na ndiyo maana wameshindwa kutokana na mfumo wao kuwa mbovu sana hali inayowafanya wakulima kugombania.

Aidha, Kiswaga ameziamuru kampuni zinazosambaza mbegu za pamba wilayani humo na Kiwanda cha Quton kinachozalisha mbegu bora za zao hilo aina ya MO8, kuanza mara moja kuuza mbegu hizo kwa wakulima na kuacha kugawa bure kutokana na kuwepo kwa mahitaji makubwa ya mbegu kwa wakulima.

Akitoa agizo hilo Kiswaga, amesema hadi kufikia Jumatatu ya wiki ijayo, kampuni hizo na kiwanda hicho wawe wameanza kuuza mbegu huku akiitaka Bodi ya Pamba kuweka utaratibu sahihi wa kuanza kuuzwa kwa mbegu hizo.

“Uamuzi huu umefikiwa kutokana na Bodi ya Pamba kushindwa kugawa mbegu kwa wakulima kwa wakati sahihi, kupitia mfumo wake mpya wa kutoa bure mbegu hizo kwa wakulima, huku yakiwepo malalamiko mengi ya wakulima kuhitaji mbegu hizo.

“Hali ya upatikanaji wa mbegu ni mbaya kwa wakulima, Bodi ya Pamba imeshindwa kuleta mbegu.

“Kama Mkuu wa Wilaya na mwakilishi wa Rais, siwezi kukaa kimya huku wakulima wakiteseka, bodi hawana uwezo hata kidogo wa kugawa mbegu, siwezi kukubali hali hii, nayataka makampuni yauze pamba kwa wakulima kuanzia Jumatatu wiki ijayo,” amesema Kiswaga.

Kiswaga amesema hadi sasa bodi hiyo imesambaza mbegu tani 2,400 huku mahitaji halisi yakiwa tani 4,000 kwa wilaya hiyo, ambapo hata hivyo mbegu hizo zilizoletwa wakulima wamepewa kidogo kulingana na mashamba waliyonayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles