NA TUNU NASSOR – DAR ES SALAAM
OFISA Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA)amezitaka Jumuiya za maji kuruhusu wateja wapya kuunganishwa maji kwa mkopo ili kuwaunganisha wateja wengi zaidi.
Kauli hiyo ameitoa leo wakazi wa ziara ya kutembelea miradi ya jamii aliyoifanya katika kata za Makangarawe, Kitunda na Mzinga.
Amesema Dawasa itawasaidia jumuiya hizo kwa kuwajengea mitambo ya kusafisha maji
Ili maji wanayotoa yawe safi na salama
“Tutawajengea mitambo ya kutibu maji(Treatment plant) ili maji yanayokwenda kwa wananchi yawe safi na salama na hivyo kusaidia kusambaza yakiwa safi na salama,” amesema Luhemeja.
Ameongeza kuwa mamlaka hiyo imeanza kuzitembelea Jumuiya za maji zilizopo katika eneo la huduma ili kuzitatua baadhi ya changamoto zinazowakabili na kuzijengea uwezo kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi.