27.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Dawa feki za mil 11/- zakamatwa

1Na Asifiwe George,

Dar es Salaam

BARAZA la Famasia nchini limekamata dawa zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 336 toka katika maduka ambayo hayajasajiliwa na kati hizo dawa zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 11 hazifai kwa matumizi.

Akizungumza wakati akikabidhi dawa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda zenye thamani ya Sh milioni 294 zilizokamatwa  Katika maduka hayo,  Msajili wa baraza hilo, Elizabeth Shakalaghe alisema operesheni ya kukamata dawa hizo ilifanywa katika mikoa tisa.

Shakalaghe alisema  dawa zilizokamatwa na zinazofaa kwa matumizi zitasambazwa katika hospitali zote za mkoa wa Dar es Salaam na kwamba tayari zimehakikiwa.

Alisema katika Mkoa wa Dar es Salaam yamefunguliwa majalada 10 kwa wale waliokamatwa na dawa za serikali ambayo kwa sasa yapo katika hatua za upelelezi.

“Bado kumekuwa na ongezeko la maduka ya dawa ambayo yanaanzishwa kinyume na sheria na taratibu hususani katika Mkoa huu na tumebaini kwamba maduka yaliyofugwa wakati wa operesheni yanafunguliwa wakati wa usiku na kuendelea kutoa huduma za dawa”alisema.

Alisema lengo la operesheni hiyo lilikuwa ni kuwabaini na kuwachukulia hatua stahiki watakaobainika kuvunja sheria ya famasia katika uendeshaji na utoaji wa huduma za dawa nchini.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa dawa hizo, Makonda alisema wamiliki wa maduka ya dawa ambao hawana vibali wanatakiwa kufunga maduka hayo Mara moja au kuzirudisha walikonunua.

Pia alivitaka vyombo vya dola na watendaji wa ngazi ya mkoa , manispaa, kata na mitaa kuhakikisha wanayafunga na kuyaondoa maduka yote ambayo hayana vibali na yanayoendeshwa kinyume na sheria ya famasia.

Hata hivyo alivitaka vyombo vya dola kufanya operesheni nyakati za usiku ili kuwabaini na kuwachukulia hatua stahiki wale watakaokaidi maagizo ya awali na kufanya biashara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles