26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Dar Musica kujitambulisha kwa mbili mfululizo

MUSICANA MWALI IBRAHIM

BENDI ya muziki wa dansi ya Dar Musica inatarajia kuachia nyimbo zao mbili mpya hivi karibuni, wakiamini kwamba nyimbo hizo zitawatambulisha vema katika muziki wanaoufanya.

Bendi hiyo mpya inayoongozwa na aliyekuwa kiongozi wa bendi ya Mashujaa Musica ‘Wanakibega’, Jado Fidforce, kwa sasa ipo kambini jijini hapa ikijifua kwa ajili ya ujio huo.

Nyimbo zitakazoachiwa hivi karibuni ni ‘Chozi la masikini’ na ‘Bongo Michongo’ ambazo zitatambulishwa kwa mashabiki wake wapya.

“Nyimbo hizo ni miongoni mwa nyimbo ambazo zitakuwa kwenye albamu yetu ambayo bado tunaiandaa na baada ya kukamilika tutazitambulisha kwenye vituo mbalimbali vya redio,” alisema huku akiongeza kwamba bendi hiyo ina wanamuziki 15 Watanzania na Wakongo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles