29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

Prezzo amtambulisha mpenzi mpya

PrezzoNAIROBI, KENYA

NYOTA wa muziki nchini Kenya, Jackson Makini ‘CMB Prezzo’, amemtambulisha mpenzi wake mpya kupitia akaunti yake ya Instagram.

Msanii huyo kwa sasa anajulikana kwa jina la ‘Mfalme Mswati’ kutokana na tabia yake ya kubadilisha wasichana kila baada ya muda.

Siku za hivi karibuni msanii huyo alionekana kuwa mtulivu tofauti na miaka iliyopita, ambapo msanii huyo alikuwa na sifa ya kugombanisha warembo, lakini kwa sasa amekuwa na aina mpya ya kubadilisha wasichana kila wakati.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, msanii huyo amemtambulisha mpenzi wake, Michelle Yola, maarufu kwa jina la Cookie na kudai kwamba huyo ndiye wake wa kudumu kwa sasa.

“Ninaamini mara baada ya mwaka mmoja nitakuita mke wangu, najua huu ni mwanzo wa uhusiano wetu, lakini mpaka kufikia mwakani nitakuita mke wangu,” aliandika Prezzo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles