26.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Dalili ubongo wa binadamu kutumika kwenye teknolojia

NEW YORK, MAREKANI

MFANYABIASHARA wa Marekani, Elon Musk amezindua nguruwe aliyempa jina Gertrude akiwa na chipu ukubwa wa sarafu ya duara kwenye ubongo wake kuonesha azma yake ya kufanikisha mpango wa mashine zinazofanyakazi kwa kutumia ubongo.

“Ni mfano wa bangili ya mkononi ndani ya fuvu la kichwa yenye nyaya ndogo mno,” bilionea huyo amesema kupitia mtandao.

Musk amesema kuwa chipu kama hizo huenda hatimae zikatumiwa kama tiba kwa magonjwa mfano wa dementia, ugonjwa wa kutetemeka mwili na majeraha ya uti ya mgongo.

Gertrude ni mmoja kati ya nguruwe watatu walioshiriki uzinduzi wa Ijumaa.

Alichukua muda kuanza kutembea lakini alipokula na kunusa nyasi, grafu iliyokuwa inatumiwa kufuatilia mienendo yake ilianza kuonesha utofauti.

Na pia alionekana kupuuza kila kitu kinachomzunguka.

Kifaa ndani ya ubongo wake kinatuma taarifa kuashiria shughuli zinazoendelea katika mfumo wa fahamu kwenye pua yake akitafuta chakula.

“Ni kifaa kinachowekwa vizuri ndani ya fuvu la kichwa. Kinaweza kuwekwa chini ya nywele na huwezi kujua.”

Kuwezesha ubongo wa binadamu kuwasiliana na mashine sio lengo rahisi

Kampuni yake ya Neuralink, inayoshughulika na utumiaji wa teknolojia na mbinu za kisasa kuingilia utendakazi wa ubongo, ilisema kwamba itaanza kufanya majaribio kwa binadamu.

Usanifu huo utawezesha watu wenye matatizo yanayosababishwa na mfumo wa neva kudhibiti simu au kompyuta kwa kutumia akili zao.

Lakini lengo lake la muda mrefu ni kukaribisha enzi ambayo Musk anaiita “utambuzi wa nguvu usio ya kibinadamu”.

Watu wanahitajika kujumuisha akili bandia au isiyo ya asili, amesema, kama sehemu ya kuhakikisha hakuna tukio la akili bandia linakuwa na nguvu, inaharibu nguvu ya binadamu.

Kwa nini wanasayansi wanataka kudukua ubongo wa mwanadamu?

Kampuni ya Neuralink iliundwa 2017, na imekuwa ikijitahidi kusajili wanasayansi kiasi kwamba hadi mwezi uliopita, Musk alikuwa bado anatangaza nafasi za kazi hizo katika mtandao wa Twitter.

Lengo la kampuni hiyo ni kutafuta mbinu za kuchochea ubongo wa mwanadamu aliyepooza kuwawezesha kudhibiti tarakilishi

Kifaa kinachotengenezwa na kampuni hiyo kinajumuisha chombo kidogo cha kukusanya habari chenye elektrodi 3,000 zilizoambatanishwa kwenye nyuzi nyembamba zaidi ya nywele za binadamu ambazo zinaweza kufuatilia chembe za mfumo wa ubongo.

Kampuni hiyo ilisema ilikuwa imefanya vipimo kwa nyani ambaye aliweza kudhibiti kompyuta kwa kutumia ubongo wake.

Pia imetengeneza roboti itakayofanya upasuaji katika ubongo ambayo inaweza kuweka elektrodi 192 kwenye ubongo kila dakika.

Profesa msaidizi wa chuo kikuu cha Pittsburgh kutoka kituo cha tiba na urekebishaji, Jennifer Collinger alielezea kile ambacho Musk alikuwa anajaribu kufanya kama “kinatatiza teknolojia wakati wa kipindi kigumu cha teknolojia ya kitiba”.

“Neuralink ina raslimali za msingi na ni kundi muhimu sana la wanasayansi, wahandishi na madaktari wanaofanyakazi kwa ajili ya lengo moja, kunakowapa fursa nzuri ya kufikia mafanikio,” alisema.

Lakini aliongeza: 

“Hata kukiwa na rasilimali hizi, uvumbuzi wa vifaa vya kimatibabu huchukua muda na usalama unahitajika kupewa kipaumbele, kwahiyo ninashuku kwamba mchakato huo utachukua muda mrefu zaidi kuliko vile ambavyo walikuwa wamesema kama malengo yao.”

Ari Benjamin, kutoka maabara ya Kording, Pennsylvania, ameiambia BBC uwa kizuizi hasa cha teknolojia kinaweza kuwachangamoto kubwa kwa ubongo wa binadamu.

“Wakishafanikiwa kuwezesha mawasiliano kati ya ubongo na mashine, kampuni ya Neuralink siku moja itafumbua fumbo la uelewa wa namna ubongo unavyoweza kufanyakazi haijalishi ni chembe ngapi za neva watakazorekodi.

“Malengo ya kutafsiri ubongo sio rahisi ikiwa hauelewi mfumo wa neva ambapo ufasiri wote unafanyika.”

Kampuni ya Musk ya anga za mbali ya SpaceX na ya Tesla zimefanikiwa kuvutia umma katika majaribio ya kuleta maendeleo kwenye nyanja ya anga za mbali na magari ya kutumia umeme.

Lakini miradi yote hiyo inaonesha tabia ya mfanyabiashara huyo ya kutangaza maazimio ya malengo makubwa ambayo huishia kuchukua muda mrefu kukamilika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles