25.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 29, 2022

Contact us: [email protected]

YANGA KUMEKUCHA

NA MOHAMED KASSARA-DAR ES SALAAM

KILELE cha wiki ya Klabu ya Yanga, maarufu Wiki ya Mwanachi, kimepangwa kuwa leo kwa tamasha litakalofanyika Uwanja wa Mkapa jijini hapa, huku kikosi cha timu hiyo kikitarajiwa kushuka kwenye dimbani kupimana ubavu na Aigle Noir ya Burundi.

Tamasha hilo linalofanyika kwa msimu wa pili mfululizo, baada ya kuzinduliwa mwaka jana, lengo likiwa kuwapa nafasi wapenzi na mashabiki wa klabu hiyo kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii.

Pia kilele cha wiki hiyo hutumika kuwatambulisha wachezaji watakaoitumikia timu hiyo katika msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara na mshindano mengine.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk.Jakaya Kikwete, anatarajia kuwa mgeni wa heshima katika tamasha hilo ambalo pia litapapambwa na burudani ya muziki kutoka kwa wanamuziki mbalimbali wakiongozwa na Harmonize. Wengine ni Bilnas, Juma Nature, Chegge, G Nako na Mzee wa Bwax

Uzinduzi wa wiki hiyo ulifanyika Agosti 22 jijini Dodoma.

Tamasha hilo limepewa jina la ‘Kubwa kuliko zote kidijitali’.

Baada ya kushindwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa misimu mitatu mfululizo, uongozi wa Yanga, umeamua kufanya usajili wa wachezaji wapya wenye viwango vikubwa, lengo kurudisha heshima yao.

Miongoni mwa wachezaji wapya wanaotarajiwa kutambulishwa leo sambamba na wale walioitumikia timu hiyo msimu uliopita ni Tuisila Kisinda, Tonombe Mukoko, waliosajiliwa kutoka klabu ya AS Vita ya DRC, Carlos Carlinhos(Inter Clube, Angola na Michael Sarpong, Ghana.

Wengine ni wazawa Bakari Mwamnyeto(Coastal Union, Yassin Mustafa(Polisi Tanzania, Waziri Junior(Mbao), Abdallah Shaibu(Huru), Kibwana Shomari(Mtibwa Sugar) na Zawadi Mauya, Kagera Sugar.

Katika kuonyesha kiu yao ya kuyashuhudia ‘majembe’ mapya mashabiki walikuwa wakijitokeza kumlaki kila mchezaji wao mpya hususani wale wa kigeni, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.


Tayari klabu hiyo imemtangaza Zlatko Krmpotic kuwa Kocha Mkuu wa kikosi hicho na jana aliwasili nchini kwa ajili ya kuanza majukumu yake hayo.

Kocha huyo raia wa Serbia, anatarithi mikoba ya Luc Eymael aliyetimuliwa baada ya kutoka matamshi ya kibaguzi kwa mashabiki wa klabu hiyo.Zlatko atasaidiana na Juma Mwambusi.

Wasanii wa filamu, akiwamo Wema Sepetu, Vicent Kigosi ‘Ray’, Jokate Mwegelo pia wamethibitisha kushiriki katika tamasha hilo.

Harmonize amejipanga vilivyo kufanya onyesho kubwa ili kumfunika bosi wake wa zamani, mwanamuzi Diamond Platnumz, ambaye alitumbuia siku ya klabu ya Simba, Simba Day.

Katika kuonyesha kupania kwake, Harmonize juzi aliwasili Uwanja wa Mkapa kwa kutumia helikopta, kwa ajili ya kukagua jukwaa atakalolitumia kutumbuiza leo.

Mkurugenzi wa Kampuni ya GSM ambayo ni wadhamini wa Yanga, Mhandisi Hersi Said alisema wamejipanga kufanya mambo makubwa kwenye tamasha hilo mwaka huu.

Sssssssssssssssssssssss

Simba kuendeleza ubabe kwa Namungo”

NA MOHAMED KASSARA

-DAR ES SALAAM

PAZIA la msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2020/21 linatarajiwa kufunguliwa rasmi leo, kwa  mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Simba na Namungo, utakaochezwa  Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Simba itacheza mchezo huo ikiwa bingwa wa msimu uliopita wa Ligi Kuu, wakati Namungo imepata fursa hiyo baada ya kufika fainali ya Kombe la Shirikisho, maarufu Kombe la Azam, kisha kukamata nafasi ya pili baada ya ubingwa kunyakuliwa na Wekundu hao.

Mchezo huo pia unazikutanisha timu zitakazoiwakilisha Tanzania katika michuano ya kimataifa, Simba ikishiriki Ligi ya Mabingwa na Namungo Kombe la Shirikisho.

Simba ilinasa tiketi hiyo baada ya kushinda taji la Ligi Kuu Bara,wakati Namungo ilimaliza nafasi ya pili Kombe la Shirikisho.

Utaratibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),unaeleza kuwa timu itakayoshinda ubingwa wa Ligi Kuu itashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na itakayotwaa Kombe la Shirikisho itakata tiketi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Lakini ikitokea timu iliyotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ndio ile ile iliyotwaa Kombe la Shirikisho, basi mshindi wa pili wa Kombe la Shirikisho atapata fursa ya kuiwakilisha nchi Kombe la Shirikisho Afrika.

Huo utakuwa msimu wa tatu mfululizo kwa Simba kucheza mchezo wa Ngao ya Jamii.Hiyo ni kutokana na kutwaa taji la Ligi Kuu mara tatu mfululizo, wakianza kuichapa Mtibwa Sugar mabao 2-1 kabla ya kuilaza Azam mabao 4-2, msimu uliopita.

Wekundu hao watakuwa wanasaka rekodi ya kutwaa kwa mara ya sita, baada ya kutwa ngao hiyo mwaka 2011, 2012,2017, 2018 na 2019.

Mchezo huo utakuwa wa nne kuzikutanisha timu hizo mwaka huu, kwani tayari zimekutana mara tatu, mara mbili kwenye ligi  na moja  Kombe la Shirikisho.

Katika kukutana huko, Simba ilishinda michezo miwili mmoja kumalizika kwa suluhu.

Mara ya mwisho zilikutana Agosti 2, mwaka huu katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela, Rukwa, Simba ilishinda mabao 2-1.

Vikosi vyote viwili vina sura mpya, Simba imefanikiwa kusajili wachezaji saba ikilenga kutikisa Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Wachezaji hao ni Joash Onyango, Ibrahim Ame, Larry Bwalya, Chris Mugalu, Benard Morrison, David Kameta na Charles Ilanfya ni miongoni mwa majina mpya yanayokwenda kuungana na kina Clatous Chama, Meddie Kagere na John Bocco msimu ujao.

Namungo nayo haiko kinyonge, imeanasa vifaa vya maana akiwemo,Shiza Kichuya, Idd Kipagwile, Sixtus Sabilo na Abdulhalim Humud.

Hata hivyo, Simba ina faida kubwa ya kutopanguka kwa kikosi chao kwa kwanza kilichofanya vizuri msimu ulioisha, huku Namungo ikilazimika kujipanga upya baada ya kuondokewa na wachezaji wao tegemeo kama Reliant Lusajo na George Makang’a.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,444FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles