26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, April 14, 2024

Contact us: [email protected]

Fursa zafunguka UAE ikisitisha kuisusia Israel

ABU DHABI, UAE

KIONGOZI wa Umoja wa Falme za Kiarabu – UAE ametoa amri ambayo inafikisha mwisho rasmi mgomo wa nchi hiyo dhidi ya Israel, kufuatia makubaliano yaliyosimamiwa na Marekani ya kurejesha mahusiano kati ya nchi hizo mbili.

Amri hiyo inafuta kabisa  sheria  namba 15 ya mwaka 1972 pamoja na  adhabu inayotokana na ukiukaji wa marufuku  hayo, kwa mujibu wa  shirika la  habari la WAM.

Muafaka huo unaoyarejesha mahusino kati ya Israel na UAE uliotangazwa Agosti 13. Uliihitaji Israel kusitisha mpango wake tata wa kuinyakua ardhi inayoikalia ya Ukingo wa Magharibi ambayo Wapalestina wanaihitaji.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo akiwa pamoja na Mfalme wa Bahrain Hamad bin Issa Al Khalifa alipotembelea Manama

Shirika la habari la serikali WAM limesema hatua hiyo ya kuondoa mgomo dhidi ya Israel imefanywa kwa amri ya Sheikh Khalifa bin Zayed Al Nahyan, mtawala wa Abu Dhabi na kiongozi wa Falme za Kiarabu. 

Amri hiyo mpya inawaruhusu Waisrael na makampuni ya Israel kufanya biashara na UAE, ambalo ni shirikisho la falme saba katika Rasi ya Uarabuni. 

Hatua hiyo pia inaruhusu ununuzi na kufanya biashara kutumia bidhaa za Israel.

Kufikishwa mwisho kwa ususiaji  huo kunaruhusu  watu binafsi  na makampuni  kufanya makubaliano na vikundi na watu binafsi ambao wanaishi nchini Israel, kuwa na uraia wa Israel ama kufanyakazi kwa niaba ya  Israel popote pale. Pia inaruhusu kuingia, kubadilishana, kumiliki na  kufanya biashara kwa kutumia  bidhaa  za Israel ndani  ya  UAE.

Israel na UAE zilitangaza makubaliano ya kurejesha mahusiano ili kupata kutoka  Israel  hatua ya kusitisha  mpango wake tata  wa kunyakua  sehemu ya eneo linalokaliwa  na Israel la Ukingo wa Magharibi.

Makubaliano hayo yanaifanya  UAE kuwa  nchi ya tatu ya Kiarabu baada ya Misri na Jordan na nchi ya kwanza ya Ghuba ya Uarabuni, kuwa  na  mahusiano ya  kidiplomasia na  Israel. 

Kumekuwa na uvumi mkubwa juu ya iwapo mataifa  mengine  ya  Kiarabu yatafuata mfano  huo.

Siku  ya  Jumatano, Waziri wa Mambo  ya  Nje wa Marekani Mike Pompeo alifanya  mazungumzo  na  Umoja wa  Falme  za  Kiarabu UAE, kama sehemu ya  ziara  yake  ya  mashariki  ya  kati, ambayo ilijumuisha  Israel, Bahrain  na  Oman.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles