29.9 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Daktari anayetuhumiwa kuomba rushwa ya ngono mjamzito Pemba asimamishwa kazi

Khamis Sharif -Zanzibar

WAZIRI wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Hamad Rashid Mohamed, ameagiza kusimamishwa kazi kwa Dk. Masoud Suleiman Abdallah wa Hospitali ya Chakechake Pemba, kutokana na kutuhumiwa kuomba rushwa ya ngono kwa mjamzito.

Hamad amesema kuwa wizara imeamua kumsimamisha kazi kwa muda wa miezi sita Dk. Masoud ili kupisha uchunguzi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Unguja, Hamad alisema kuwa Serikali imesikitishwa na tukio la daktari huyo lililotokea Novemba 21, mwaka huu akidaiwa kumwomba mama mjamzito rushwa ya ngono ndipo aweze kumtibia.

Hamad alisema SMZ kwa kushirikiana na taasisi zenye dhamana zitaendelea na uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo na pindi uchunguzi ukapokamilika taratibu za kisheria zitafuatwa.

 “Iwe ni kweli amelifanya au si kweli, Wizara ya Afya inachukizwa na matendo hayo kwani si katika maadili ya kazi na niseme kuwa si mara nyingi kwa wananchi kutoa taarifa hizi, inawezekana ipo namna, ila tusubiri uchunguzi utakapokamilika na hili litakuwa funzo kwa watumishi wengine wenye tabia mbaya na chafu kama hizo,” alisema Hamad.

Alisema jamii inatakiwa kuachana na dhana potofu ya kutowapeleka wake zao hospitali kwa kuhofia tukio kama hilo.

Novemba 23, mwaka huu Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) kisiwani Pemba, ilifanikiwa kumnasa daktari huyo akiwa anataka kufanya rushwa ya ngono kwa mjamzito kisha ndipo aweze kumpatia huduma ya uchunguzi hospitalini hapo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles