20.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Kizimbani akituhumiwa kubaka mtoto wa miaka 7

Erick Mugisha -Dar es salaam

MKAZI wa Mwananyamala B, Mustafa Mohamed (36) amepandishwa kizimbani Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam kwa kosa la ubakaji wa mtoto wa miaka saba.

Mwendesha Mashtaka wa Jamhuri, Benson Mwaitenda, akimsomea hati ya mashtaka mtuhumiwa mbele ya Hakimu Simon Swai, alidai kati ya Februari 2019 na Oktoba 10, 2019 eneo la Mwananyamala Kisiwani wilayani Kinondoni, Dar es Salaam alimbaka mtoto wa miaka saba.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa na mwendesha mashtaka wa Jamhuri alidai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuomba mahakama kumsomea hoja za awali.

Mwaitenda alimsomea mshtakiwa mashtaka manne ambapo alikubali hoja tatu na kukana kosa la tatu.

 “Mshtakiwa nimemsomea hoja zote nne za awali na kukubali hoja namba moja, mbili, nne na kukataa kutenda hoja namba tatu, hata hivyo naomba mahakama tarehe nyingine kwa ajili ya kuleta mashahidi wa kesi hiyo,” alidai Mwaitenda.

Hakimu Swai alisema dhamana kwa mshtakiwa ipo wazi kwa kuwa na wadhamini wawili waaminifu wenye barua za utambulisho, nakala ya kitambulisho cha taifa na kusaini bondi ya Sh 2,000,000. 

Mshatakiwa alitimiza masharti ya dhamana na kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 28, itakapokuja kwa ushahidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,595FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles