30.7 C
Dar es Salaam
Thursday, December 19, 2024

Contact us: [email protected]

CWT Maswa wamvaa Waziri Ndalichako

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,  Profesa Joyce Ndalichako.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako.

Na SAMWEL MWANGA-MASWA

CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT) Wilaya ya Maswa Mkoa wa Simiyu kimedai kusikitishwa na kauli ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,  Profesa Joyce Ndalichako akipinga madeni ya walimu.

Akizungunza na waandishi wa habari juzi, Mwenyekiti wa CWT Wilaya ya Maswa, Onesmo Makota alisema kauli ya Prof. Ndalichako si ya kweli na inaweza kusababisha madhara makubwa kwa walimu na uchonganishi kati ya walimu na Serikali.

Alisema kwa upande wa Wilaya ya Maswa pekee walimu wanaidai Serikali Sh milioni 500 za malimbikizo ya mapunjo ya mishahara na madai yasiyo ya mishahara.

“Sisi kama chama cha walimu wilaya ya Maswa tunaipinga kauli hiyo, baada ya kujiridhisha kwa kupata taarifa kutoka ofisi za maofisa elimu msingi na sekondari kuwa walimu wa Wilaya ya Maswa wanaidai serikali madai mbalimbali yanayofikia zaidi ya Sh milioni 500, sasa anaposema Serikali haidaiwi anamaanisha nini?,”alihoji.

Akifafanua zaidi alisema malimbikizo ya mapunjo ya mishahara ni Sh 428,333,846.16 na madai yasiyo ya mishahara ni Sh 167,844,440 na kubainisha kuwa iwapo madai haya yapo na serikali imekuwa ikishidwa  kuwalipa kwa wakati walimu wake leo waziri amepata wapi ujasiri wa kueleza hayo.

Makota alisema kuwa ni vizuri serikali ikajenga nyumba za kuishi walimu kwani watakwenda wenyewe bila kusukumwa vinginevyo watawashauri wahamie madarasani na mengine hayana hata sakafu.

Naye Katibu wa CWT Wilaya ya Maswa, Emmanuel Samara alisema chama hicho kinafanya jitihada mbalimbali katika kuhakikisha Serikali inawalipa walimu madeni yao yote yaliyohakikiwa kwani yamekuwa ya muda mrefu.

“CWT Maswa haitarudi nyuma tutafanya kila jitihada mbalimbali kupaza sauti ili kuhakikisha serikali hasa ya awamu ya tano inawalipa madeni yao yote wanayodai kwa shule za msingi na shule za sekondari,”alisema.

Aidha wamewataka walimu wa wilaya hiyo waendelee kuwa wavumilivu wakati madeni yao yanashughulikiwa kwa kuongeza juhudi katika kufanya kazi kwani mustakabali wa mafanikio ya kielimu nchini upo mikononi mwao.”Wajibu na Haki” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles