23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Muhongo awapa kibano wakandarasi wazembe

Profesa Sospeter Muhongo
Profesa Sospeter Muhongo

Na BENJAMIN MASESE-KAGERA

SERIKALI imesema  haitawapa kazi wakarandasi nane waliokuwa waliokuwa wakitekeleza miradi ya Wakala wa Umeme Vijijini (REA), kutokana na kuonesha udhaifu na kushindwa kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Kauli hiyo imetolewa juzi na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, alipokuwa akizungumza  na wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) mkoani Kagera.

Profesa Muhongo alisema Serikali haiweze kuendelea kufanya kazi na wakandarasi wazembe  wasiofikia malengo kwa kuwa wanakwamisha juhudi za Rais Dk. John Magufuli za kutaka kuwaondolea matatizo wananchi walioteseka kwa miaka mingi.

Bila kuwataja wakandarasi na kampunin zao, Profesa Muhongo alisema, tayari Serikali imefanya upembuzi wa wakandarasi waliotimiza wajibu wao wakati wa utekelezaji wa REA awamu ya pili na kubaini wakandarasi nane hawakufikia malengo yaliyokusudiwa.

“Tunayo majina ya wakandarasi nane ambao kazi zao hazikuturidhisha,  walishindwa kufikia malengo yaliyokuwa yamewekwa na hivyo hatutathubutu kuwapa kazi tena katika REA awamu ya tatu, tukiendelea kufanya kazi na watu wa aina hii Serikali haitafikia lengo lake la kuwaondolea wananchi changamoto za kukosa nishati hii ambayo ni muhimu katika uchumi wa wakazi wa vijiji.

“Kama Serikali tuwahakikishie wananchi kwamba vijiji vyote nchini vitakuwa vimepata huduma ya umeme katika kipindi cha miaka mitano kupitia Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III), kwani tayari zimetengwa Sh trilioni moja kwa ajili ya shughuli hiyo,  fedha nyingi kuliko zilizowahi kutengwa,”alisema.

Profesa Muhongo alisema  utekelezaji wa  REA awamu ya tatu utakuwa na kasi kubwa  na Serikali itahakikisha  unakamilika kwa wakati kama ilivyokusudiwa huku akiwatahadharisha wakandarasi watakaopewa mradi huo kufanya kazi kwa bidii.

Katika hatua nyingine, Profesa Muhongo aliwaasa wafanyakazi hao wa Tanesco kujiepusha na vitendo vya rushwa  au kutengeneza mazingira  yanayoweza kusababisha ufanisi wa kazi kutokuwapo.

Hata hivyo katika kuonyesha dhamira hiyo ya kuepuka rushwa, wafanyakazi hao walikula kiapo mbele ya Profesa Muhongo  na kuahidi kwamba hawatajihusisha na vitendo vya rushwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles