28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

CRDB yapata faida ya Sh bilioni 236

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Benki ya CRDB imepata faida ya Sh bilioni 236 kabla ya kodi kwa mwaka 2020 ikiwa ni ongezeko la asilimia 35 kulinganisha na Sh bilioni 175 iliyoripotiwa mwaka 2019.

Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Abdulmajid Nsekela, ameelezea mabadiliko yanayoendelea ambayo yameongeza uwezo wa benki katika kutoa huduma huku yakichochewa pia na mazingira mazuri ya biashara.

“Licha ya changamoto za COVID-19, tulipata ahueni mkakati wetu wa kusaidia wateja wakati wa janga hili ulituwezesha kurekebisha mipango yetu,” amesema Nsekela.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akizungumza wakati wa kutangaza faida ya benki hiyo kwa mwaka 2020, Kulia ni Ofisa Mkuu wa Fedha, Fredrick Nshekanabo.

Amesema mapato yasiyo ya riba yameongezeka kwa asilimia 13 hadi Sh bilioni 284 bilioni kutoka Sh bilioni 252 zilizoripotiwa 2019.

Aidha, amesema amana za wateja zilikua hadi Sh trilioni 5.4 kutoka Sh trilioni 5.2 zilizoripotiwa mwishoni mwa 2019.

“Faida tuliyopata imechangiwa zaidi na kampuni tanzu mbili ambazo zilichangia asilimia 7. CRDB Burundi ilifanya vizuri licha ya changamoto zilizotokea Burundi.

“Faida ya Kampuni tanzu ya Burundi ilikua kwa asilimia 75 kutoka Sh bilioni 6.4 hadi Sh bilioni 11.2. Kampuni tanzu ya bima (CRDB Insurance Broker Limited) ilirekodi faida ya Sh bilioni 3.6 ikiwa ni ukuaji wa asilimia 140 kwa mwaka,” amesema Nsekela.

Mkurugenzi huyo amesema mikopo ya vikundi na maendeleo ilikua kwa asilimia 16 hadi Sh trilioni 3.9 ikilinganishwa na Sh trilioni 3.4 trilioni zilizoripotiwa 2019.

Kuhusu rasilimali za benki amesema zimeongezeka kwa asilimia 9 hadi kufikia Sh trilioni 7.2 kulinganisha na Sh trilioni 6.6 iliyoripotiwa 2019.

Naye Ofisa Mkuu wa Fedha (CFO), Fredrick Nshekanabo, amesema walihakikisha mikopo inakuwa na afya licha ya changamoto wanazokumbana nazo wateja wao na kwamba Mikopo isiyolipika (NPL) ilipungua kwa asilimia 4.2 kutoka asilimia 5.5 iliyoripotiwa 2019.

“Tunaendelea kufuatilia na kufanya kazi kwa karibu na wateja wetu katika sekta zilizoathiriwa na janga hili,” anasema Nshekanabo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles