23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Hivi ndivyo utakavyojua uwezo wa dawa inayokutibu

Na Aveline Kitomary, Mwanza

Mchunguzi wa dawa kutoka Mamlaka ya Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi (TMDA) Kanda ya Ziwa, Kapilia Lameck amesema maabara hiyo inachunguza uwezo wa dawa katika kutibu ugonjwa.

Lameck amesema mashine ya kisasa inayoitwa, High Performance Liquid Chromatragraphy (HPLC) inauwezo wa kugundua kama kiambata hai kilichopo kwenye dawa ni sahihi na kinauwezo wa kutibu ikiwemo dawa asili.

Lameck amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari waliofanya ziara maalum katika maabara ya mamlaka hiyo iliyoko jijini Mwanza.

Mchunguzi wa dawa Kapiliya Lameck akionesha jinsi mashine HPLC inavyopima dawa

Hapa anafafanua zaidi; “Mashine hii inaanza na kupima uzito ili kuangalia kama dawa tunayopima ni ile inayokidhi vigezo vilivyowekwa.

“Katika dawa kuna layer zingine kama vibebeo kuna wakati mwingine tunaangalia ulinganifu wa uzito kutoka kidonge kimoja na kingine
na wakati wa kusajili vitu vingi vinaangaliwa ikiwemo uzito, mwonekano na mengine.

“Tunaweka dawa kwa ajili ya kuisaga baada ya hapo tunaweka kwenye mashine kwa ajili ya kuchangaya kwa dakika 20, lazima tuangalie kama kuna kiambata hai katika dawa husika,”anaeleza.

Lameck amesema mashine hiyo ya HPLC inauwezo wa kusoma dawa husika kwa kulinganisha na kiwango kilichowekwa kimataifa kwani wapo waliosajiliwa kitaifa kutengeneza dawa za mbalimbali na zimehakikiwa.

“Hivyo tunakuwa na dawa ya kulinganisha nayo kama kulinganisha kwa dawa zingine na HPLC inapima dawa ili kuweza kusoma dawa husika kwa kuangalia viwango vya dawa inayotakiwa kimataifa, hivyo baada ya maandalizi na upimaji kusoma.

“Katika soko la dawa kuna mambo mengi kama kutibu mtu na biashara, mtu mwingine anaweza kufanya udanganyifu ili kupunguza gharama hivyo sisi hapa tunahakiki hii inaonesha kama kuna kiambata hai kwenye dawa au hamna,”amebainisha.

Amesema katika upimaji wanatumia kemikali ambazo zimeelekezwa katika miongozo hivyo mashine inapokuwa inafanya kazi na kemikali zinakuwa zinapita katika mifumo ya mashine.

“Kwenye hii mashine kuna sehemu inabeba pampu ambayo inapanda na kushuka una’set’ unasubr inafanya kazi yenyewe hadi ulipo’set’ itaishia mahali kila kitu kimetenganishwa mpaka tupate kile tunachotaji.

“Mashine hii Inauwezo wa kupima dawa zaidi ya mmoja zinasomeka katika wavelate ina ‘plate’ mbili na kwenye ‘computer’ lazima uoneshe unameweka kwenye plate ipi hii inasaidia wakati wa kusoma na inafanya kazi kama roboti lazima useti,”ameeleza.

Amefafanua kuwa mashine hiyo inaweza kufanya kazi muda mrefu kwa kutumia umeme; “Unaweka jenereta automatic unaweza kuweka hata aina 20 za dawa,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles