30.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Craver Tz arudi kivingine na ‘Ubongo’

NA CHRISTOPHER MSEKENA

BAADA ya kufanya vizuri na wimbo, Mzobe Mzobe, msanii wa Bongo Fleva kutoka Uyole jijini Mbeya, Venance Mahenge Craver Tz, amerudi kivingine na Ubongo, ngoma mpya ya mapenzi yenye ubunifu wa hali ya juu.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Craver ambaye ametoka Mbeya kuja Dar es Salaam kupambania muziki wake alisema ngoma hiyo mpya ni jibu kwa mashabiki waliokuwa wanasubiri wimbo mpya.

“Nipo tofauti na wasanii wengi wa hapa Mbeya kuanzia aina ya muziki wangu, tungo mpaka uimbaji kwa sasa nimekuja hapa Dar mimi na mshkaji wangu Bizy Boy kwaajili ya kusambaza ngoma hii ambayo nimetoa audio na video na tayari inachezwa kwenye redio, Tv na ipo kwenye chaneli yangu ya YouTube na kikubwa ambacho ninaomba ni sapoti,” alisema Craver.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles