TURIN, ITALIA
MCHEZO wa mzunguko wa pili (marudiano) hatua ya nusu fainali ya Coppa Italia kati ya wenyeji Juventus dhidi ya AC Milan umehairishwa kutokana na hofu ya kuenea kwa virusi vya ugonjwa wa Corona nchini HUMO.
Uamuzi huo umetolewa baada ya amri ya Waziri Mkuu kuainisha vizuizi vilivyowekwa katika hafla za michezo nchini kote hadi Machi 8, mwaka huu.
Mchezo huo wa marudiano ulipangwa kuchezwa jana bila mashabiki kutoka mikoa iliyoathiriwa zaidi, lakini badaye ulisogezwa mbele.
Hatua hiyo imetokana na mkutano ulihudhuriwa na Meya wa Turin Chiara Appendino, Claudio Paolomba, wawakilishi wa klabu na wizara za mitaa Jumanne.
Italia imeamua kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa huo tishio duniani kwa sasa ambao tayari umeshaua watu zaidi ya 3,000 kote ulimwenguni tangu ulivyolipuka nchini China mapema mwaka huu.
Taarifa ya Juventus ilisema: “Mchezo huo umeahirishwa kwa tarehe ambayo bado haijathibitishwa, kama ilivyotangazwa na Lega Serie A, baada ya kuchukua hatua kutoka kwa agizo la Jimbo la Turin n.14801 / 2019 / Area1 la 3 Machi 2020, ambalo ilitolewa baada ya mkutano wa leo [Jumanne] kumaliza. ”
Ripoti za vyombo vya habari sasa zinadai kuwa serikali ya Italia inazingatia kuahirisha hafla zote za michezo kwa mwezi mmoja ili kupunguza athari za ugonjwa huo.
Wakati huo huo,
Wizara ya afya nchini Hispania imeliambia shirikisho la soka nchini humo kuamuru
michezo ya Ligi YA Mabingwa Ulaya na ile ya
Europa Ligi kufanyika bila ya
mashabiki kufuatia hofu ya kuenea kwa ugonjwa wa Corona.
.
Mechi hizo zitakazochezwa bila ya mashabiki ni
dhidi ya klabu za Italia ambazo zinatoka nchini humo kunakodaiwa kuwa ugonjwa
wa Corona tayari umeingia na umeshasababisha michezo kadhaa kuhairishwa.
.
Mechi ya marudiano ya klabu bingwa kati ya
Valencia dhidi ya Atalanta itachezwa bila ya mashabiki.
.
Pia mechi kati ya Getafe dhidi ya Inter Milan ya
michuano ya Europa Ligi itachezwa bila
ya uwepo wa mashabiki.