ROTTERDAM, Uholanzi
POLISI nchini Uholanzi wamelamizika kutumia nguvu ya ziada kuwakabili raia wanaopinga hatua ya Serikali kuweka katazo la kutoka nje (lockdown) ili kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona.
Katika maandamano hayo, imeripotiwa kuwa polisi wamewaua kwa risasi watu wawili mjini Rotterdam, ambako kulishuhudiwa matukio ya vurugu za kurusha mawe na kuchoma moto magari ya wanausalama hao.
Hatua ya Serikali ya Uholanzi kuja na mkakati wa ‘lockdown’ ya wiki tatu ilitokana na kasi kubwa ya maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo.
Mbali ya watu wawili kuuawa na wengine saba kujeruhiwa, wapo 20 wanaoshikiliwa na polisi kwa kuhusika katika vurugu hizo.