27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 12, 2024

Contact us: [email protected]

Tolisso agombewa Spurs, Inter

MUNICH, Ujerumani

KUNA vita nzito inayoendelea kati ya Tottenham, Inter Milan na Juventus, ambapo klabu hizo zinashindana kumsajili staa wa Bayern Munich, Corentin Tolisso.

Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 27, atakuwa mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu, hivyo Bayern wanaona ni bora kumuuza Januari, mwakani, kuliko kumwacha aondoke bure.

Tolisso si mchezaji muhimu kwa Bayern kwani msimu huu ameingia mara moja pekee kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Julian Nagelsmann.

Alijiunga na Bayern mwaka 2017 akitokea Lyon lakini majeraha ya mara kwa mara yamemzuia kuwa kwenye kiwango chake cha juu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles