NEW YORK, Marekani
WATU zaidi ya milioni tano wameshapoteza maisha tangu ugonjwa wa Corona ulipoanza miezi 19 iliyopita na hiyo ni kwa mujibu wa takwimu za Chuo Kikuu cha Johns Hopkins.
Katika utafiti wake, Chuo Kikuu hicho kimebaini kuwa watu takribani milioni 250 duniani kote wamepata maambukizi vya vurusi vya ugonjwa huo, huku ikitiliwa shaka kuwa huenda idadi ni kubwa zaidi.
Marekani ni kinara baada ya watu wake zaidi ya 745,800 kufariki dunia, ingawa Shirika la Afya la Kimataifa (WHO) linaamini idadi ya vifo vya Corona duniani ni kubwa mara tatu ya iliyotajwa.
Kwa takwimu zilizopo, ambazo wataalamu wa afya wanasema idadi ya vifo vya majumbani haipatikani, Brazil inafuata kwa vifo vingi, 607,824, huku nafasi ya tatu ikishikwa na India yenye watu 458,437 waliopoteza maisha.