Nairobi, Kenya
Rais Uhuru Kenyatta amezifunga kaunti tano nchini Kenya kutokana na ongezeko la wagonjwa wa corona.Kaunti hizo ni Nairobi, Kajiado, Machakos, Kiambu na Nakuru.
Marufuku hiyo inaanza ifikapo saa sita usiku.
Hakuna usafiri wa barabarani,angani na reli utakaoruhusiwa kuingia na kuondoka katika sehemu hizo zilizotajwa kama zenye janga ‘kubwa la corona’.
Maeneo hayo yatakuwa chini ya masharti hayo ya zuio kwa siku 30 zijazo.
“Ukiwapima Corona Wakenya 100, basi 20 watapatikana na virusi hivyo. Kiwango cha maambukizi kimezidi mara kumi zaidi,” amesemaRais Kenyatta.
Rais Uhuru amesema wimbi la tatu la janga ilo nchini Kenya linatarajiwa kufika kilele chake katika siku 30 zijazo. s