25.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

COCA-COLA KUTENGENEZA KINYWAJI CHENYE BANGI

WASHINGTON, MAREKANI

KAMPUNI maarufu ya vinywaji ya Coca-Cola, ambayo inafahamika zaidi kwa utengenezaji wa soda, sasa inapanga kutengeneza aina mpya ya kinywaji chenye bangi.

Kwa mujibu wa mtandao wa habari wa BNN Bloomberg wa hapa, kampuni hiyo itashirikiana na kampuni mwenyeji ya utengenezaji bangi ijulikanayo Aurora Cannabis.

Lengo kuu la kuwa

..na kinywaji hicho kitakachoanza kwa majaribio litakuwa ni kupunguza maumivu na si kulewesha watu.

Kampuni hiyo, bado haijazungumzia hadharani mpango huo lakini imekiri inafuatilia kwa karibu sekta ya vinywaji vyenye bangi.

“Kwa pamoja na wadau wengine wengi katika sekta hii ya vinywaji, tunafuatilia kwa karibu ukuaji wa soko la vinywaji vyenye bangi aina ya cannabidiol visivyolewesha kama kiungo katika vinywaji vya kuboresha afya maeneo mengi duniani,” taarifa ya Coca-Cola imesema.

Cannabidiol, ni moja ya viungo vinavyopatikana ndani ya bangi, na inaweza kusaidia kupunguza kuvimba, maumivu na kuganda kwa misuli na huwa haileweshi.

Hatua hiyo, imechangia kuibuka kwa biashara kubwa ya ukuzaji wa bangi, pamoja na kuundwa kwa ushirikiano wa kampuni kubwa katika biashara hiyo.

Mapema mwaka huu, kampuni kubwa ya utengenezaji wa bia ya Molson Coors Brewing ilitangaza kutengeneza vinywaji vyenye bangi kwa ushirikiano na kampuni ya Hydropothecary, huku kampuni inayotengeneza bia ya Corona, Constellation Brands, ikiwekeza zaidi ya dola bilioni nne katika kampuni ya bangi ya Canopy Growth.

Ushirikiano kati ya Coke na Aurora utakuwa ni kisa cha kwanza kabisa kwa kampuni kubwa ya uzalishaji wa vinywaji visivyolewesha kujiingiza katika biashara aina hiyo.

BNN Bloomberg, wakinukuu vyanzo vya habari, ambavyo havikuwa tayari kutajwa, wamesema Coca-Cola wanafanya mazungumzo ‘yenye uzito’ na Aurora lakini kufikia sasa hawajapata maafikiano yoyote.

Mazungumzo yamepiga hatua na maafikiano yanakaribia kupatikana, mdokezi mmoja alinukuliwa akisema.

“Itakuwa ni katika kitengo cha vinywaji vya kuponya au kumpa mtu ahueni,” mdokezi huyo ameongeza.

Aurora, kupitia taarifa wamesema hawataki kuzungumzia mipango yao ya kibiashara hadi ikamilishwe.

Lakini aliongeza: Aurora wameeleza hamu yao kuu kutumia fursa ya kibiashara katika vinywaji vyenye vileo, na tunakusudia kuingia katika soko hilo.”

Bangi hutokana na mmea wenye kemikali aina ya tetrahydrocannabinol (THC), ambayo huathiri akili za mtu na kumfanya ajihisi vyema, jambo linalowafanya baadhi kuitumia wakiamini itawasaidia kupunguza mawazo.

Lakini pia inaweza kuwafanya watu kuwa na njozi mbaya na wasiwasi usio wa kawaida.

Husababisha uraibu, na asilimia 10 ya watumiaji wa kawaida wa bangi huwa waraibu.

Cannabis pia huwa na cannabidiol (CBD), ambacho ndicho kiungo Coca-Cola wanatarajiwa kutumia.

Wanasayansi wamekuwa wakichunguza matumizi ya kiungo hicho kama dawa.

Tiba za kutumia CBD zimeonyesha mafanikio makubwa katika kupunguza athari za kifafa, hasa kwa watoto.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles