24.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 27, 2024

Contact us: [email protected]

Chuo Kikuu cha Ibadan Nigeria chaonyesha utayari kushirikiana na Tanzania

Abuja, Nigeria

Chuo kikuu cha Ibadan, Nigeria, chaonesha utayari wa kushirikiana na vyuo vya Tanzania katika kufundisha Kiswahili.

Dhamila hiyo imebainishwa wakati wa ziara ya, Balozi Benson Alfred Bana chuoni hapo, Mei 10, 2022.

Pamoja na mambo mengine, Balozi alifanya ziara hiyo kuushukuru Uongozi wa Chuo Kikuu cha Ibadan kumtunuku Shahada ya Udaktari wa Heshima Mwl. Julius Kambarage Nyerere nwaka 1979, ikiwa ni kutambua mchango wa Mwalimu katika mambo mbalimbali pamoja na ukombozi wa Bara la Afrika, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 100 ya Mwl. Nyerere.

Aidha, ziara hiyo imeweka msingi wa kujadili na kuona namna chuo hicho kinavyoweza kuanzisha uahirikiano na vyuo vya Tanzania hasa katika kufundisha somo la Kiswahili.

Makamu Mkuu wa Chuo cha Ibadan, Prof. Kayode Adebowale alimshukuru Balozi Bana kwa ziara hiyo na akahidi kuwa chuo cha Ibadan kipo tayari kwa namna yoyote ile kushirikiana na vyuo vya Tanzania katika kufundisha Kiswahili pamoja na masuala mengine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles