27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 12, 2024

Contact us: [email protected]

Chuo cha IAA chajipanga kutoa elimu kwa njia ya mtandao

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Chuo cha Uhasibu Arusha(IAA), kimejipanga katika utoaji wa elimu kwa njia ya mtandao ngazi ya Shahada ya Uzamili.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Chuo hicho, Dk. Cairo Mwaitete wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya maonesho ya NaneNane ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Mbeya.

Amesema, awali chuo hicho kiliaanza kutoa elimu hiyo kwa njia ya mtandao baada ya kuingia ugonjwa wa Uviko-19.

Amesema, baada ya hapo walibaini kuwa wanafunzi wengi wanauhitaji wa kuongeza elimu lakini changamoto inayowakabili ni muda, hivyo chuo kikaamua kuendelea na njia hiyo ya utoaji wa elimu kwa njia ya mtandao ili kulisaidia kundi hilo.

“Wakati wa elimu hii ya mtandao inaanza changamoto ilikuwa kwa wanafunzi wa Certificate na Diploma ambao walikuwa hawana uwezo wa kukununua vifurushi ila kwa kundi la shahada ya uzamili likifanya vizuri na ndio sababu tumeamua kuendelea nao ambapo sasa watalazimika kusoma ndani ya mwaka mmoja tu,” anasema.

Hata hivyo, akizungumzia uhusiano wa kilimo cha biashara na chuo hicho, amesema chuo kimejiandaa vyema na utoaji wa elimu kwa wakulima kwani kilimo cha biashara ni lazima kiendane na elimu ya uhasibu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles