24 C
Dar es Salaam
Thursday, July 25, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaombwa kuboresha miundombinu Uwanja wa Nyamhongoro

Na Sheila Katikula, Mwanza

Serikali imeombwa kuboresha miundo mbinu kwenye uwanja wa Nyamhongoro ili wafanyabiashara waweze kuepuka gharama za maandalizi ya maonyesho.

Kauli hiyo imetoa leo Agosti 8, 2022 na Meneja Masoko wa Kampuni ya Tanzania China inayojishughulisha na uuzaji wa piki piki za mataili mawili na matatu, Makoye Kayanda wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya nane nane yanayofanyika kwenye uwanja wa Nyamhongolo uliopo Wilayani Ilemela mkoani Mwanzo.

Amesema inaskitisha kuona gharama za kulipia maonyesho zinatolewa na mfanyabiashara lakini miundo mbinu siyo rafiki na maandalizi ya kujenga mabanda hufanywa na mfanyabiashara kwa fedha zao.

“Tunaomba tuboreshewe miundo mbinu ya kwenye uwanja huu ambao unatumika kwenye maonyesho ya nane nane miaka yote kwani tunalipia fedha za kupewa eneo ambalo tutaweka bidhaa zetu lakini unatakiwa ujenge banda kwa fedha zako na kutumia fedha nyingi za maandalizi.

“Nimelipa sh milioni moja kwa ajili ya kupata eneo la kuweka bidhaa zangu lakini unatumia fedha nyingi za maandalizi ya eneo tofauti na gharama ya maonyesho kwani inapelekea kupata hasara.

“Eneo hili lilikuwa na majani na matuta nimetumia fedha nyingi kusawazisha
tunaomba serikali iweke utaratibu wa kutoa eneo ya kudumu kwani inaskitisha kuona mwaka huu nimeandaa eneo kwa fedha nyingi alafu mwakani anapewa sehemu nyngine,”amesema Makoye.

Hata hivyo ameiziomba taasisi za kifedha kuweka huduma za kibenki ili waweze kutoa na kuweka fedha na siyo kutoa elimu ya kutunzaji wa fedha tuu kwa wateja wapya.

Ameishukru serikali kwa kuweka ulinzi wa kutosha kwenye eneo hilo kwani wafanyabiashara wanafanyaka kazi zao bila wasi wasi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles