23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Christina Tossy atoa siri ya ‘Ameniona”

Na Mwandishi Wetu, Mtanzia Digital

MWIMBAJI wa nyimbo za Injili nchini, Christina Tossy, amesema wimbo wake mpya wa Ameniona umebeba ushuhuda wa maisha yake.

Akizungumza na Mtanzania Digital leo Jumatano, Novemba 24, 2021 Christina amesema pamoja na changamoto alizopitia anamshukuru Mungu kwa kuendelea kumpigania na kumwonyesha watu sahihi na wasio sahihi kwenye huduma na familia yake.

“Namshukuru Mungu ameendelea kutushika mkono na kutuvusha katika vipindi mbalimbali vigumu mimi na familia yangu, mfano Juni mwaka huu nilimpoteza mama yangu mzazi kwa hiyo kupitia vile nikajua watu sahihi na watu wasio sahihi maana hao wasio sahihi walichukua mali zote za mama.

“Hata hivyo, namshukuru Mungu kwa kuruhusu nimpoteze mama ili nijue kuwa wale ndugu wa mama hawakuwa ndugu halisi pia nimekubali hiyo hali na ninaendelea na maisha yangu, wimbo upo kwenye chaneli yangu ya YouTube ya Christina Tossy,” amesema mwimbaji huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles