30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Chriss Brown: Mashabiki wananiumiza kichwa

chris-brownNEW YORK, MAREKANI

MKALI wa muziki wa RnB nchini Marekani, Chris Brown, amesema kwamba anafanya muziki mzuri kwa kuwa huwa anawafikiria zaidi mashabiki wake kabla ya kuandika mashairi.

Msanii huyo kwa sasa yupo katika mgogoro na Nia Guzman, aliyezaa naye mtoto (Royalty), kwa madai kwamba anamsababisha ugonjwa wa pumu mtoto huyo kutokana na matumizi ya sigara anazovuta Chris Brown.

“Tangu nimepata mtoto kikubwa ambacho ninakifikiria ni mwanangu na mashabiki wanataka nini katika nyimbo zangu, hali hii imekuwa tofauti na miaka ya nyuma kabla sijapata mtoto.

“Mashabiki wananifanya nitumie muda mwingi kutengeneza muziki wenye viwango, kikubwa mashabiki wanataka burudani na ndicho ninachokifanya kila siku,” alisema Chris.

Hata hivyo, msanii huyo amedai kwamba tangu amempata mtoto huyo maisha yake yamebadilika kwa kuwa sasa anaishi maisha ya kiutu uzima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles