27.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 5, 2023

Contact us: [email protected]

Jay Z amshtaki Rita Ora

Ora_M_1769698aNEW YORK, MAREKANI

KAMPUNI ya kurekodi muziki ya Jay Z, Roc Nation, imemshtaki mwanamuziki Rita Ora ikidai kwamba amevunja mkataba wake wa makubaliano kwa kutotengeneza idadi ya albamu alizoahidi.

Hata hivyo, Rita amedai kwamba mikataba ya kampuni hiyo ni haramu, hivyo ameomba kujitoa.

Msanii huyo alijiunga na kampuni hiyo akiwa na umri wa miaka 18 na sasa ana miaka 25, alikuwa miongoni mwa wanamuziki wa kwanza kusajiliwa na Jay Z.

Kutokana na hali hiyo, kampuni ya Roc Nation imesema itataka ilipwe dola milioni 2.4 kwa kuwa imetumia zaidi ya dola milioni 2 kutengeneza na kuiuza albamu ya msanii huyo ambayo haijatoka.

Makubaliano ya msanii huyo na kampuni ya Roc Nation ni kwamba atengeneze albamu tano chini ya Kampuni hiyo, lakini hadi sasa ametengeneza albamu moja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles