27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Chris Brown, mama mtoto hapatoshi

chris-brown-y-royalty-610x600NEW YORK, MAREKANI

BAADA ya mkali wa muziki wa RnB nchini Marekani, Chris Brown kushinda kesi ya kumlea mtoto wake Royalty wiki iliyopita dhidi ya mama mtoto wake, Nia Guzman, kwa sasa wawili hao wameanza kurushiana maneno.

Mrembo huyo alimshitaki Chris kwa madai kwamba ana malezi mabaya kwa mtoto huyo kama vile kuvuta sigara mbele yake na mambo mengine mengi, lakini kwa sasa msanii huyo ameshinda kesi hiyo hivyo Nia ameanza kumshambulia kwenye mitandao ya kijamii.

“Ninaamini mwanangu ataishi katika maisha ambayo sikuyatarajia, nadhani kuna mchezo umechezeka ili Chris ashinde kesi hiyo ila natambua kwamba mwanangu atateseka,” aliandika Nia.

Hata hivyo, Chris naye aliamua kumjibu mrembo huyo kwa kusema kwamba, mtoto mwenyewe anapenda kuishi maisha anayoishi yeye mwenyewe na hakuna mambo mabaya ambayo anayafanya kwa sasa.

“Royalty anafurahia maisha yake, niliamua kubadilika na kuwa baba bora ili nimuweke katika mazingira mazuri, ninashukuru kwa sasa nimebadilika na mtoto ataishi vizuri,” aliandika Chris.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles