25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

CHINA YAUA MAJASUSI 20 WA MAREKANI

NEW YORK, MAREKANI


GAZETI la New York Times la hapa limeripoti kuwa China, imewaua au kuwafunga jela majasusi kati ya 18 na 20 wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita na kudhoofisha kabisa shughuli za kulichunguza taifa hilo kubwa la Asia.

Gazeti hilo liliwakariri maofisa 10 wa zamani na sasa wa Marekani, ambao waliomba majina yao kuhifadhiwa wakati wakilaani kitendo cha karibuni cha kuvujisha siri za kijasusi kwa Urusi kilichofanywa na Rais Donald Trump.

Walisema kitendo hicho ni ukiukaji mbaya wa kiusalama zaidi kipindi cha miongo kadhaa.

Walikumbushia vitendo kama hivyo vya uvujishaji siri vilivyoangamiza maisha ya majasusi na watoa habari wa Marekani nchini China, hali iliyopelekea kusambaratika kwa mtandao wake nchini humo.

Baadhi ya maofisa hao wanasema wanadhani China, ilidukua mfumo wa mawasiliano wa CIA, ambao hutumiwa katika mazungumzo ya siri.

Lakini wengine wanaoamini kulikuwa na mdukuzi ndani ya CIA aliyesambaratisha kizuizi cha siri cha wapelelezi wa Marekani mwaka 2010.

Ripoti ya gazeti hilo na Associated Press inasema idadi ya mali za CIA zilizopotea nchini China haitofautiani na zile zilizopotea wakati wa uliokuwa Umoja wa Kisovieti (USSR) na Urusi kutokana na usaliti uliofanywa na afisa wa CIA Aldrich Ames na kachero wa Shirika la Upelelezi Marekani (FBI), Robert Hanssen, ambao walikamatwa mwaka 1994 na 2001.

Majasusi wa CIA nchini China walianza kutoweka mmoja baada ya mwingine kuanzia mwanzoni mwa 2011 huku mmoja wao akipigwa risasi mbele ya wenzake katika eneo la kupumzikia katika jengo la serikali mjini Beijing.

Hata hivyo, CIA imekataa kuzungumzia suala hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles